Marquee
tangazo
Thursday, May 20, 2010
ABDALLAH ALLY MTOLEA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA C.U.F TEMEKE
ABDALLAH ALLY MTOLEA ATANGANZA NIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI
ABDALLAH ALLY MTOLEA
ABDALLAH ALLY MTOLEA
ABDALLAH ALLY MTOLEA ALIPOKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI DAR ES SALAAM LEO
ABDALLAH ALLY MTOLEA AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI EBEN-EZERY MENDE WA TAFAKARI
ABDALLAH ALLY MTOLEA
ABDALLAH ALLY MTOLEA KATIKA PICHA YA KIPANDE
ABDALLAH ALLY MTOLEA AKIWA AMEPOZI
ABDALLAH ALLY MTOLEA AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI sAIDI MWISHEE WA JAMBO LEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH; ABDALLAH ALLY MTOLEA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI-CUF
Mimi Abdallah A Mtolea ambaye ni kijana wa miaka 34 na ni Mwanachama wa chama cha CUF Amechukuwa fomu ya kugombea Ubunge ndani ya chama chake akisuburi mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hiko ambao unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 11 juni 2010 hadi 10 julai 2010 amechukuwa fomu katika tawi lake la Changamoto lililopo Yombo BUza katika kata ya Makangarawe tarehe 13 machi 2010 na amefata taratibu zote za chama chake na kuirejesha katika ofisi ya Wilaya CUF Temeke kwa muda muhafaka.Pamoja na kuwa mimi ni mwanachama wa CUF, lakini pia kitaaluma mimi ni muhuitimu wa shahada ya kwanza ya sheria kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam mwaka 2009, na nimewai kufanya kazi katika kampuni ya simu za mkononi ya Celtel/Zain na HITS kati ya mwaka 2001 hadi 2008 na 2008 hadi 2009 kwa nafasi mbalimbali. mwaka 2010 niliamua kuachana na kazi nza ajira na kujishughulisha na biashara ili nipate muda mweingi wa kutosha wa kuitumikia jamii na kufanya shughuli za kisiasa.nimeamua kuwania nafasi hii ya Ubunge katika jimbo la Temeke baada ya kuona kuwa huduma za jamii zinazidi kudidimia na kuongezeka kwa matatizo katika nyanja zote za kijamii zikiwemo ,ELIMU,AFYA,MIUNDOMBINU,UCHUMI na kudorora kwa harakati za kimaendeleo kwa ujumla, kunatokana na mipango yake ni ya kisiasa zaidi kuliko kuangalia maslai ya wananchi na maendeleo kiujumla ya wana Temeke. mipango wanayoiweka katika kutatua kero hizi imekosa ubunifu kabisa
Kwa kutumia Elimu yangu, Utafiti wangu dhamira yangu ya dhati kushughulikia kero za wananchi na rasilimali tulizonazo katika manspaa ya Temeke na kwa kushirikiana na Madiwani,wataaramu wetu na wananchi wakaazi wa Temeke naimani katika kipindi hiki kifupi kijacho endapo nitafanikiwa kuwa mbunge wa jimbo hili tayari tumetoa mwerekeo wa kupunguza matatizo na kero hizo kama sio kuzitokomeza kabisa.
Ni matarajio yangu kuwa wananchi wa Temeke tutaungana pamoja kupata mtu stahiki anaye tambua kero na matatizo yetu lakini pia mwenye mikakati madhubuti ya kukabiriana nayo,MbunifuMsomi na ambaye ni mkazi wa Manspaa yetu na wala sio mtu aneyetoka nje ya eneo letu ambaye kwa vyovyote vile awezi kuwa na uchungu na maendereo yetu kama ilivyo maeneo mengi.
Ni vema WAnanchi wa TEmeke watambue kuwa mimi nini sifa hizo
Nawajulisha pia wananchi wote wa Temeke watambue uwepo wangu katika kuwania nafasi hiyo muhimu ya kimaamuzi katika nchi kwa kupitia katika mchakato wa kupata mgombea ndani ya chama changu ambacho ndicho kitakachokuwa dira ya kutimiza thabiti na mikakati yake ya ujenzi wa nchi hii
Ahsante sana nawatakia kila la kheri kazi njema
Abdallah Ally Mtolea
abdalah ally Mtopea akiwa na Rajabu mhamila super D katika mikutano yake na waandishi wa habari DAr es salaam leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment