Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 26, 2010

ZANTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA ZPESA ZANZIBAR


Wateja wa Zantel Zanzibar wakijiandikisha kwa ajiri ya kutumia huduma za ZPesa baada ya kuzinduliwa upya Zanzibar juzi. Uzinduzi huu unaambata na zoezi la kusajili namba za simu
za mikononi kabla ya tarehe 31, Juni 2010.(Picha na Mpigapicha wetu)


Waziri wa Nchi wa Zanzibar anayesimamia maswala ya Fedha na Uchumi Bw.Mwinyihaji Makame akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa upya wa huduma ya ZPesa nchini Zanzibar juzi. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Bw.Noel Herrity na Afisa Mkuu wa Kibiashara wa Zantel Bw.Norman Moyo.(PIcha na Mpicha picha wetu)

Zantel yazindua ZPesa Zanzibar
NA Mwandishi wetu
Zanzibara

KAMPUNI ya simu za mikononi ya Zantel imezinduwa huduma yake ya kibenki kupitia simu za mkononi ijulikanayo kama Zpesa kwa wakazi wa Zanzibar.

Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Bw. Noel Herrity alisema Zantel imeona kuna umuhimu wa kuleta karibu huduma za kibenki kwa wananchi walio wengi ambao hawapati huduma za kibenki lakini wana simu za mikononi.

Alisema huduma hiyo yenye mtazamo mpya imeongezewa huduma mpya zitakazowawezesha wateja wa Zantel nchini Zanzibar kulipia na kukunua bidhaa tofauti kama umeme, maji, tiketi za ndege, kulipia DSTV pamoja na kununuwa muda wa maongezi mbali ya kutuma na kupokea fedha.


“Zantel tunafahamika kama kampuni yenye ubunifu ambayo inajitahidi kuwawezesha Watanzania kupata huduma za mawasiliano zilizo nafuu na katika mfano huu wa ZPesa tunawaletea wateja wetu huduma za kibenki haswa wale ambao hawana fursa ya kupata huduma hizo,” alisema Bw. Herrity.

Uzinduzi mpya wa ZPesa unaenda sambamba na shughuli za kusajili namba za simu kuwawezesha wateja wa Zantel kuandikisha namba zao kabla ya tarehe 31 Juni, 2010.

Wateja wa Zantel watakaojiunga na huduma ya ZPesa moja kwa moja namba zao zimesajiliwa na watapata bonus ambao ni hela itakayowekwa kwenye akaunti yao ya Zpesa au wanaweza kuchukuwa muda wa maongezi kupitia wakala wowote wa ZPesa.

Naye Ofisa Mkuu wa Kibiashara Bw.Norman Moyo alisema kuwa Zantel imewahusisha wafanyabiashara, vyama pamoja na makundi yenye wanachama waliosambaa sehemu mbalimbali nchini kuwa mawakala wa Zpesa.

“Zantel inawawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo kukuza biashara zao kwenye maeneo ambao hayajafikiwa na huduma za kibenki pamoja na kuwaongezea kipato. Vyama pamoja na makundi mbalimbali pia yataweza kupata kipato cha ziada ambacho kitawasaidia wanachama wao pamoja na kuendesha shughuli za chama au kikundi,” alifafanuwa Bw. Moyo.

Uzinduzi mpya wa ZPesa utafanyika nchi nzima ukianzia na Zanzibar kabla ya kuhamia mikoa mingine. Huduma ya ZPesa inapatikana nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...