Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 22, 2010

Casillas achekelea Valdes kuitwa kikosi cha Hispania


Casillas achekelea Valdes kuitwa kikosi cha Hispania

MADRID,Hispania

MLINDA mlango wa timu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya Taifa ya Hispania, Iker Casillas amesema kwamba kuitwa mlinda mlango wa Barcelona, Victor Valdes katika kikosi kitakachokwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia ni uamuzi mzuri.

Casillas, ambaye jana alitimiza umri wa miaka 29 tangu mwaka 2002 amekuwa mlinda mlango namba moja lakini akasema kuwa mafanikio aliyoyapata katika mechi 102 alizochezea timu ya Taifa kikubwa ni ubingwa na akasema kuwa atahakikisha anapambana kama wachezaji wengine ili kuhakikisha analinda nafasi yake.

Alisema kuwa vilevile walinda mlango wawili Diego Lopez na David De Gea ambao wamekosa nafasi katika kikosi cha mwisho chenye wachezaji 23 wana uwezo wa kutosha kwenda Afrika Kusini.
"Ni uamuzi sahihi . Wachezaji wote watano waliokuwemo katika kikosi cha awali wangeweza kwenda lakini kocha akaamua kubaki na hawa watatu ambao anadhani ni bora na sasa sote tutapigania nafasi kuwemo katika kikosi cha kwanza,"mlinda mlango huyo alikaririwa na Shirika la Habari la Hispania AS akisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...