Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 31, 2010

WANACHAMBA SIMBA WAMTAKA ADEN RAGE


Na Benedict Kaguo,Tanga

WANACHAMA wa Klabu ya Simba Mkoani Tanga wamemtaka Mwenyekiti mpya wa Klabu hiyo,Ismail Aden Rage ametakiwa kufanya ziara za mara kwa mara Mkoani Tanga ili kuwamasisha wanachama kujiunga na klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao,Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoani hapa,Mbwana Msumari alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wanachama katika mkoa huo.

Msumari alisema wanachama wa klabu hiyo Mkoani hapa wanaimani kubwa na
Mwenyekiti huyo mpya wakiamini kuwa atasaidia kuiwezesha klabu hiyo
kujizolea sifa katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Hadi sasa klabu ya Simba Mkoani Tanga ina jumla ya wanachama hai,850
kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga.

Msumari aliongeza kuwa kwa sasa kuna jumla ya wanachama wapya 278 ambao
wameomba uachamana katika klabu hiyo ambapo ikiwa Mwenyekiti huyo mpya
atatembelea Mkoani hapa ataongeza chachu ya kuongeza idadi ya wanachama
wapya..

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...