Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 23, 2010

RIADHA TAIFA WANANGWA NA WADAU,KISA ETI WANAENDEKEZA MSHIKO BILA KUJALI UHAI MCHEZO WENYEWE

RIADHA TAIFA WANANGWA NA WADAU,KISA ETI WANAENDEKEZA MSHIKO BILA KUJALI UHAI MCHEZO WENYEWE

Na Moses Ng’wat,
Mbeya.

WADAU wa mchezo wa riadha mkoa wa Mbeya wamekitupia lawama chama cha Riadha Tanzania (RT), kwa kushindwa kutoa programu za maendeleo ya mchezo huo kwa timu za mikoani ambapo wangeibuka wachezaji chipukizi wa kulisaidia taifa , badala yake wamekuwa waking’ang’ania kuandaa mashindano ya Taifa.

Wakizungumza jijini hapa, wadau hao walisema kwamba wanashangazwa na uongozi wa riadha taifa kutangaza tarehe ya mashindano ya taifa kwa mwaka huu bila kuwa na uhakika wa uhai wa vyama vinavyosimamia mchezo huo katika mikoa na wilaya.

Hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari jijijini Dar es Salaam , Katibu MKuu wa RT, Mujaya Selemani Nyambui, alitangaza kuwa michuano ya taifa ya mchezo huo yanatarajia kufanyika Juni 25 hadi Juni 27 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mmoja wa wadau hao Rashidi Kasiga aliponda namna chama hicho kushindwa kuendesha shughuli zake kisayansi ili kiweze kutoa matokeo bora,badala yake imeng’ang’ania kuendesha mashindano ya Taifa kwa lengo la kuvuna fedha za wadhamini.

Mtindo huo wa uendeshaji mchezo ho kamwe hautatoa matokeo mazuri na badala yake Tanzania itaendelea kupeleka wachezaji wasio na uwezo katika michuano ya kimataifa na kupata matokeo yanayolitia aibu taifa.

Lakini pia alisema uendeshaji huo unachangia kuua mchezo huo ambao katika miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa juu kwa kuchuana na mataifa ya Kenya ,Ethiopia,Morroko na Maifa mengine ambayo yapo katika ubora katika viwango vya ubora wa mchezo huo kimataifa.

“Hawa jamaa kazi zao ni za kukurupuka,mwaka jana baada ya kumalizika mashindano ya taifa tulitegemea wangetembelea mikoa kuhamasisha ili mwaka huu wachezaji wakaonyeshe viwango vyushindani, lakini matokeo yake hakuna kilichofanyika” alihoji Kasiga.

mbeya

Wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira waendelea kusotea mishahara

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...