Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 23, 2010

DK.NAGU AZUSHA BALAA MBEYA ILA MAPAMBANO YANAENDELEA

DK.NAGU AZUSHA BALAA MBEYA


Na Moses Ng’wat,
Mbozi.mbeya,

ZIARA ya waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu, mkoani Mbeya imeingia shubiri baada ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Aden Mwakyonde na Ofisa mtendaji wa mamlaka ya mji Tunduma ,Aidan Mwashinga kujikuta katika wakati mgumu baada ya umati wa wananchi wa Tunduma kuzomea mbele ya waziri huyo.

Tukio hilo lilitokea juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Chama cha Mapinduzi (CCM ),kata ya Tunduma ,baada ya viongozi hao kutoa majibu yaliyoonekana kuwa ni ya hovyo kwa wananchi baada ya waziri kuulizwa swali na yeye kutoa fursa kwa viongozi hao kujibu.

Swali lililozua balaa kwa viongozi hao ,liliulizwa na mfanyabiashara Esto Sinka ambaye alitaka kujua ni kwanini waziri huyo anasisitiza ufufuaji wa viwanda ili hali viongozi hao wamekuwa wakiendesha oparesheni za kunyanganya na kupora baiskeli za wananchi katika mji huo kwa kisingizio kuwa zinasababisha uchafu.

“Ndugu waziri umezungumzia uimarishaji wa biashara za mpakani kama hapa kwetu, pamoja na kufufua na kuendeleza viwanda vya hapa nchini,lakini cha ajabu baiskeli zetu zinaporwa eti ni ni uchafu sasa kwanini unaendelea kuhubiri mambo yanayosababisha kero kwa jamii” alihoji Sinka.

Kufuatia swali hilo, waziri Nagu alimtaka Ofisa mtendaji wa mji huo wa Tunduma Aidan Mwashinga kutoa majibu,lakini akiwa katikati ya kutoa majibu wananchi walilipuka kwa makelele na kuanza kuzomea kwa nguvu wakimtaka aondoke mbele ya waziri kwa madai kuwa majibu aliyokuwa akiyatoa hayakuwa na ukweli wowote.

Hata hivyo wananchi hao walipaza sauti wakitamka maneno atoke ,atoke wameuza eneo letu “hata huyo diwani anayetaka kusimama naye ni walewale hawana jipya la kutueleza”, na kusababisha diwani huyo Aidani Mwakyonde ambaye ni mwenwa halmashauri ya wilaya ya Mbozi kuamua kurudi kukaa kwenye kiti.

Lakini, waziri Nagu aliingilia kati kwa kuwaambia wananchi hao kuwa wasikivu kwa kuwa serikali ya CCM ni sikivu na ipo kwa ajili ya wananchi na kwamba kero hiyo itatatuliwa ili kujenga misingi bora ya kuwapatia wananchi huduma.

Hata hivyo Dk.Nagu aliendelea na jitihada zake za kuwapoza wananchi hao walioonekana wenye jazba na akawaeleza kuwa kuwa waziri akishapokea malalamiko si rahisi kutoa majibu hadharani lakini kile kilichoelezwa na wananchi kitafanyiwa kazi ili kupunguza misuguano na kuweka mazingira mazuri kwa kila mwannanchi kufanya shughuli zake za halali bila bughuza.

Wakizungumza baada ya mkutano huo wafanyabiashara hawa wanaotumia baiskeli kuvusha mizigo ya wafanyabiashara wanaotoka Tanzania na kuingia nchini Zambia walidai kuwa viongozi hao wa mji mdogo waliuza eneo walilotengewa awali kwa ajili ya kuegesha baiskeli hizo lakini baadaye eneo hilo liliuzwa na wao kupelekwa sehemu ambayo hailingani na mazingira ya kazi zao.

Hali iliyowalazimu kuingia mitaani na kukutana na dhahama ya ubabe wa kunyang’anywa baiskeli zao ambazo ni vitendea kazi muhimu katika shughuli zao za ubebaji mizigo.

Mwenyekiti wa halimashauri hiyo Aden Mwakyonde ambaye pia ni diwani wa kata ya Tunduma alidai kuwa vijana hao wa baiskeli ni wakorofi kwa kuwa hawataki kuhamia katika maeneo waliopangiwa na kusababisha msongamano na kukiri kuwa oparesheni za kupora baiskeli zilifanyika ambapo hadi sasa halmashauri hiyo inashikiria baiskeli sita.

Mwisho.

Na Moses Ng’wat,
Mbozi.

Tatizo la ujenzi holela wa nyumba bila kuzingatia mipango miji, katika mji wa Tunduma uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambi umesababisha udhibiti wa biashara za magendo kuwa mgumu.
Imedaiwa kuwa udhaifu huo wa kutokuwa na miundo mbinu mizuri ya ujenzi katika makazi ya miji ya mipakani imekuwa ikitumiwa na wafanyabiashara wengi kutorosha bidhaa na kuisababishia serikali kukukosa mapato stahili.

Hayo yalibainika juzi katika risala ya mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo aliyoisoma kwa kwa waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu katika moja ya ziara zake mkoani hapa ,alipotembelea wilaya hiyo.

``Mheshimiwa Waziri ujenzi holela na usio wa mpango wa nyumba katika miji yetu ya mpakani unaendelea kuwa kikwazo na changamoto kubwa kwa serikali kuweza kukusanya mapato yake vizuri,`` alisema Kimolo.

Aidha, Kimolo alimueleza waziri huyo kuwa kukosekana kwa soko la pamoja la mpakani kwa wananchi wa nchi hizo mbili za Tanzania na Zambia ni moja ya matatizo ambayo yanasababisha kushindwa kudhibitiwa kwa biashara ya njia za panya.

Alisema changamoto nyingine inayochangia uendelezaji wa biashara za magendo katika mpaka huo ni bidhaa za Tanzania kuendelea kuuzwa kwa bei ya juu ukilinganisha na bidhaa za nchini Zambia kama sukari.

Akizungumzia sababu iliyochangia kushindwa kudhibiti ujenzi holela katika mpaka huo ni kuondolewa kwa alama za mpakani (Becons),hali iliyosababisha ujenzi wa makazi kuingiliana kati ya miji ya Tunduma nchini Tanzania na Nakonde nchini Zambia.
Waziri huyo wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu amekuwa katika ziara ya siku tatu katika mkoa wa Mbeya kwa kutembelea katika wilaya ya Mbeya, Mboozi na Kyela na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara jambo lililotafsiriwa kuwa ziara za kisiasa na si za

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...