Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 29, 2010

Vitali Klitschko kumvaa Sosnowski leo akishinda kupambana na David haye


Vitali Klitschko kumvaa Sosnowski leo

GELSENKIRCHEN, Ujerumani

BINGWA wa ngumi wa uzito wa juu Duniani wa WBC, Vitali Klitschko leo anatarajiwa kutetea ubingwa wake, dhidi ya Albert "The Dragon" Sosnowski.

Mzaliwa wa Ukraine, "Dr. Iron Fist" Klitschko, ambaye anaishi Hamburg, ataingia ulingoni katika uwanja wa Veltnis Arena mjini Gelsenkirchen akiwa na rekodi ya 41-2 (37 KO).

Sosnowski, ambaye ni mzaliwa wa Warsaw anayeishi Brentwood, England, ana rekodi ya 45-2-1 (27 KO).
Licha ya Sosnowski kuwa na rekodi nzuri katika miaka yake 12 ya kucheza ngumi za kulipwa, bingwa huyo wa zamani wa Ulaya haonekanani kama ni mahiri sana katika ngumi za uzito wa juu.

Sosnowski, ambaye ni mfupi zaidi akilinganishwa na Klitschko, ameachana na kupigania mkanda wa ubingwa wa Ulaya akitaka kuwania ubingwa wa Dunia.
Bado, Klitschko hamdharau mpinzani wake Sosnowski.
"Ninatarajia Albert Sosnowski atakuwa katika kiwango kizuri katika maisha yake," Klitschko alisema.
"Alisema atafanya kila kitu, ili kuweza kumchukua mkanda wangu, lakini nimejiandaa vizuri, lakini pia nimejiandaa vizuri na sitamdharau. Atakuwa na nguvu na kila wakati atakuwa akisonga mbele. Atafanya kila kitu kutaka kutwaa ubingwa."
Kocha wa Klitschko, Fritz Sdunek alitamba kuwa mteja wake yuko kwenye kiwango ambacho si cha kawaida na amejifuanza kupiga ngumu kali kwa ajili ya pambano hili.
"Kwa mara nyingine tena, amekuwa bora katika kupigana," Sdunek alisema. "Amefanya kazi sana kwa ajili ya miguu yake na alicheza zaidi ya raundi 110 za sparring,"
Klitschko alipoteza mechi mbili kutokana na kuumia ya kwanza ilikuwa dhidi ya Chris Byrd na nyingine dhidi ya Lennox Lewis. Klitschko hadi pambano linasimamishwa alikuwa akiongoza kwa pointi.

Sosnowski amerejea ulingoni baada ya kumtwanga, Danny Williams katika raundi ya tisa Novemba, 2008 na kisha alitoka sare na Francsesco Pianeta wa Italia katika mechi ya kuwania ubingwa wa.

Katika mechi yake ya mwisho, Sosnowski alitwaa ubingwa wa Ulaya kwa kushinda kwa pointi dhidi ya Paolo Vidoz wa Italia.

"Nimejiandaa vizuri na kuja hapa kutengeneza historia. Klitschko atanizuia mimi nafasi," Sosnowski alisema.

Sosnowski anatumaini kufanya vizuti katika mechi ya leo, ambayo inatarajiwa kutazamwa na mashabiki kiasi cha 40,000 mjini Gelsenkirchen.

Klitschko amekuwa na mtazamo wa kupigana na bingwa wa WBA, David Haye katika mechi yake ijayo, ambaye awali hakuweza kupigana na kaka yake bingwa wa IBF and WBO, Wladimir Klitschko.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...