Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 23, 2010

Ngassa azitaka ubaya Simba, Yanga MPAKA KIELEWEKE


Ngassa azitaka ubaya Simba, Yanga

Na Mohamed Akida

KAULI ya kwanza ya mshambuliaji mpya wa Azam FC, Mrisho Ngassa itakuwa inatangaza vita mpya kwa klabu yake ya zamani pamoja na mahasimu wao wakuu wa Simba.

Ngassa alisema kutokana na dau kubwa alilonunuliwa na timu yake mpya ya Azam atahakikisha kuwa anakuwa mchezaji bora kulingana na dau lake na kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kuipa ubingwa timu yake.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa alinunuliwa na Azam kwa sh. milioni 58 ikiwa pamoja na dau la usajili wa sh. milioni 40 na mshahara wa milioni 1.4 kwa mwezi.

"Nimenunuliwa kwa pesa nyingi lazima nifanye kazi zaidi ya niliyokuwa nikifanya Yanga na zawadi kubwa kwa timu yangu ni ubingwa na naamini hilo litawezekana kama tukiwa na ushirikiano," alisema Ngassa.

Ngassa ambaye amekabidhiwa jezi namba 16 kama aliyokuwa akivaa Yanga, alisema amefurahi kuichezea Azam kwa dau kubwa lakini anaamini kuwa anakazi ngumu mbele yake ya kuipaisha timu hiyo msimu ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye makeke mengi uwanjani aliongeza: "Azam ni moja kati ya timu iliyokuwa ikifanya vizuri hata msimu uliopita lakini naamini kwa kikosi kitakachokuwa nacho msimu ujao Simba na Yanga wasahau ubingwa.

Kwa upande wake Kocha msaidizi wa timu hiyo, Habibu Kondo alisema wamefurahi kumnasa Ngasa kwani nia yako kubwa ilikuwa ni kuimarisha kikosi chao ili kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa msimu ujao.

Kondo alisema wanamatarajio makubwa na Ngassa na wanaamini atawasaidi kwa uwezo wake wote ili kuweza kuipaisha timu hiyo ambayo msimu uliopita ilikamata nafasi ya tatu.

Ngassa ni mchezaji watatu kusajili na Azam katika kipindi hiki baada ya kumsajili kipa Jackosn Chove na mshambuliaji wa Polisi ya Uganda, Peter Senyonjo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...