Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 29, 2010

MSHAMBURIAJI WA TIMU YA TAIFA YA HISPANIA FERNANDO TORRES KUWA FITI WAKATI WA FAINAL ZA KOMBE LA DUNIA


Torres awapa matumaini Hispania

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Hispania, Fernando Torres atakuwa fiti wakati wa fainali za Kombe la Dunia, baada ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza na timu hiyo tangu afanyiwe upasuaji.

Juzi Torres alifanya mazoezi kwa muda wa dakika 45, sambamba na wachezaji wenzake 22, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana uwanjani, tangu afanyiwe upasuaji huo kwenye goti la mguu wake wa kulia Aprili 18, mwaka huu.

“Ni habari njema Fernando kujiunga nasi mazoezini. Kwetu sisi ni mchezaji muhimu na magoli yake ni muhimu sana,” alisema beki wa timu hiyo, Gerard Pique. “Natumaini atakuwa tayari kwa mechi ya ufunguzi ya Kombe la dunia,” aliongeza.

Hadi sasa mshambuliaji huyo wa Liverpool, tayari ameichezea timu hiyo ya taifa ya Hispania, mara 72 na kuifungia mabao 23 likiwemo bao lililoifanya timu hiyo, kutwaa ubingwa wa fainali za Mataifa ya Ulaya mwaka 2008, mbele ya Ujerumani.

Mbali na Torres mchezaji, Cesc Fabregas naye pia alifanya mazoezi na timu hiyo, huku kiungo huyo wa Arsenal akiendelea kupona mguu wake uliovunjika.

Katika fainali hizo, Hispania imepangwa kundi H ikiwa na timu za Uswizi, itakayokutana nayo Juni 16 kabla ya kuzikabili Honduras na Chile.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...