Marquee
tangazo
Wednesday, May 19, 2010
KAMPUNI YA BIMA YA RESOLUTION HEALTH YAZINDULIWA KWA MAFANIKIO
Waziri Mkulo akipokea Zawadi ya kujirinda wakati wa Uzinduzi wa kampuni ya bima
Wakurugenzi wa bodi wakiwa katika picha ya pamoja na waziri Mkulo
Wadau mbalimbali wakiwa katika ufunguzi uho
Waziri akiongea na waandishi wa habari
Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo wa pili kushoto akilsalimiana na Balozi Ally Karume Dar es salaam juzi walipokutana wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya bima ya Afya ya Resolution Health itakayotoa huduma Afrika Mashariki kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Richard Kasesela
Kundi la THT rikitoa burudani wakati wa hafla hiyo jana
Waziri akisalimiana na wadau wa bima wakati wa uzinduzi wa kampuni ya bima
Bendi ya No name wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya bima ya Afya ya Resolution Health Dae es salaam juzi itakayotoa huduma Afrika Mashariki kushoto ni Simon Mukibi Fred Tranchart na Said Ali
Inocent Lameck akipanga zawadi mbalimbali kwa ajiri ya waandishi wa habari wakati wa afla hiyo
Taji Liundi kushoto akiteta na wasanii wa THT kabla ya kutumbuiza
Na Godfrida Jola
WATANZANIA wameshauriwa kujiunga na mfuko bima ya afya ili kupata huduma bora na za uhakika.
Hayo yalisemwa juzi jijini na Waziri wa Fedha na Uchumi bw.Mustafa Mkulo katika hafla ya kufungua kampuni ya Bima ya afya ya Afrika Mashariki ya Resolution Health, kuwa asilimia ya wananchi wote ndio wamejiandisha.Aliitaka kampuni hiyo kufanya utafiti ili kubaini vikwazo vya kujiunga na huduma hizo ili waweza kujiunga."Resolution life itawasaidia wananchi wengi kupata huduma za afya , pia itaongeza pato la nchi kwakua tutapata kodi toka kwao," alisema Bw.Mkulo
Naye msimamizi mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw.Dennis Lumula alisema huduma mpya zitakazotolewa malipo ni pamoja na meno, huduma kwa wajawazito na malipo ya matibabu ya papo kwa papo.
"Tumejenga zaidi ya vituo 250 afrika mashariki ili kuwahudumia watu wengi zaidi sehemu wanakoishi," alisema BW.Lumula Alisema wanachama wa kampuni hiyo hulipiwa huduma za matibabu hadi wakiwa na umri wa miaka 60 ambapo wataweza kupata huduma ndani ya nchi za tatu za Afrika mashariki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment