Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 26, 2010

KIKOSI KAMILI CHA BLAZIL KUTUA NCHINI KWA MAZOEZI


Na Zahoro Mlanzi

KIKOSI cha timu ya taifa ya Brazil chenye nyota Robinho, Kaka, Cesar, Cicinho, Maicon na Lucio, kinatarajia kutua nchini kabla ya Kombe la Dunia kujipima ubavu na timu ya taifa 'Taifa Stars' ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo.

Hayo yamezungumzwa Dar es Salaam jana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga wakati akitoa ufafanuzi juu ya taarifa mbalimbali zilizoonekana kwenye mitandao ya nje ya nchi.

Mbali na hilo, tiketi 380 kwa ajili ya kombe la Dunia tayari zimeshaletwa nchini, hivyo wadau mbalimbali ambao wamezilipia wanatakiwa wakazichukue pamoja na risiti walizokatia tiketi hizo na picha ndogo (passport size).

Tenga alisema ameamua kulizungumzia hilo la ujio wa Brazil mapema baada ya vymbo vya habari mbalimbali duniani kuanza kutoa taarifa na kwamba tayari mazungumzo yanaendelea na yamefikia hatua nzuri.

''Tumeamua kutangaza mapema licha ya kuwa bado hatujamalizana na Brazil kwa maana hatujasaini mikataba bado mpaka sasa lakini tulipofikia ni pazuri, hivyo tunachosubili ni kujua watakuja lini na wachezajhi wangapi,'' alisema Tenga.

Alisema ni wiki moja sasa tangu waanze mazungumzo na wanatarajia siku yoyote kuanzia sasa watajua timu hiyo inatua nchini lini na ni lazima iwe kabla ya kombe la dunia kuanza.

''Hakuna asiyependa kuiona Brazil ikiwa nchini na nyota kama Kaka, Robihno na wengine ila tumeshaambia kwamba tuko tayari kutimiza masharti yao watakayotuambia, na hili serikali inatia mkono kwani ni ujio wa timu kubwa,'' alisema Tenga.

Mbali na hayo, Tenga aliipongeza timu ya taifa ya Wanawake 'Twiga Stars', kwa ushindi walioupata wa mabao 8-1 dhidi ya Eritrea katika kuwania kufuzu fainali za Afrika kwani ni ushindi wa kihistoria.

Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Frolian Kaijage, alisema tiketi 380 za kombe la dunia zilizotengwa kwa ajili ya Tanzania tayari zimeshafika, hivyo wadau waliolipia tiketi hizo wanatakiwa kwenda kuzichukua.

''Tiketi zimeshafika, sasa wale waliolipia wanaweza kuja kuzichukua na si kununua kwani tiketi zote zimeshalipiwa na lile suala la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuongrza tiketi zingine za ziada kwa Juni, suala hilo linaonekana kuwa gumu kwa sasa,'' alisema Kaijage.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...