Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 18, 2010

RIADHA WAANZA MCHAKATO

CHAMA cha Riadha Tanzania (RT) kimeitaka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kutuma majina ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Taifa ya mchezo huo ifikapo Juni 20 mwaka huu.

Michuano hiyo inatarajia kufanyika Juni 25 hadi Juni 27 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu MKuu wa RT, Selemani Nyambui alisema Mikoa yote inatakiwa kutuma majina hayo ili iwe rahisi kwao kupanga bajeti ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kuandaa chakula na malazi kwa timu za mikoani.

Alisema michuano hiyo ambayo husaidia pia kupata timu ya Taifa ya riadha Tanzania kwa ajili ya kushiriki michuano mbalimbali
itaiwezesha RT kupima vipaji vya wanariadha ambao wamechaguliwa kushiriki michuano ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika New Delhi nchini India.

"Wanariadha ambao wanashiriki madola kwa upande wa mbio fupi itakuwa ni jaribio lao la kwanza la kupima vipaji vyao katika mashindano haya isipokuwa wale ambao wanakimbia mbio ndefu za Marathon ambao tayari viwango vyao vimefuzu kushiriki madola , wao watashiriki ili kulinda viwango vyao visiporomoke,"alisema Nyambui.

Alisema mashindano hayo pia yataibua vijana chipkizi ambavyo vitapata nafasi ya kuingia katika kikosi cha vijana kinachonolewa na makocha wacuba kupitia programu maalum inayofanywa na makocha hao.

Nyambui alisema bingwa mtetezi wa mwaka jana ni mkoa wa Arusha ukifuatiwa na Singida ambapo walifanikiwa kutoa wanariadha wengi katika nafasi za mwanzo.

Alisema meta zitakazokimbiwa katika mashindano hayo ni kuanzia meta 100 hadi meta 10,000 na pia kutakuwa na wanariadha watakaokimia nusu marathon.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...