MWIMBAJI mahiri wa Bendi ya Extra Bongo 'Next Level' Ally Choki amesema kutokana na kuhama hama bendi nyingi katika maisha yake ya muziki hayupo tayari kuihama bendi hiyo kwa sasa.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kambi ya bendi hiyo, iliwekwa kwa muda katika Hotel ya Trees,Dar es Salaam choki aliliambia Majira kuwa bendi yake hiyo ya sasa itadumu naye kwa muda mrefu na kama atahama basi itakuwa mipango ya mungu.
Choki ambaye siku za nyuma amewahi kuzitumikia bendi za Twanga Pepeta, TOT Plus na Mchinga Sound alisema amedhamilia kuiweka kileleni Extra Bongo ili ije kuwa moja kati ya bendi hatari katika muziki wa dansi hapa nchini.
"Jamani bendi yetu ndiyo hii Extra Bongo imekuja tena na mimi nipo hapo na safari hii sijui kama nitaondoka kama nitaondoka sijui, sijui, nimetembea katika bendi nyingi saizi nipo hapa," alisema Choki na kuangusha kicheko.
Choki aliongeza "Tunawaomba ushirikiano tufike, na niwahakikishie tu wapenzi wetu kuwa vitu vingi tumeviandaa na tunaendelea kuviandaa kaeni mkao wa kura na tutaanza kuwaonyesha katika utambulisho wetu karibuni pale Msasani Beach," alisema.
Aidha Choki ameliwataka wadau na wapenzi wa Bendi hiyo kuonyesha ushirikiano ili kuiwezesha ihimili kwa muda mrefu na isipoteze umaarufu wake hasa mara baada ya ujio wake wa mara ya pili baada ya kupoteza dira kwa muda tangu mwaka juzi.
Extra Bongo inayotamba na kibao chake cha Mjini Mipango ijumaa hii inatambulisha ujio wao mpya na baada ya kukaa kimya kwa muda wa miaka miwili na baada ya mwezi mmoja kufafuatiwa na uzinduzi wa albamu yao mpya ya Mjini Mipango.
No comments:
Post a Comment