Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 21, 2010

TIMU YA NGUMI YA ASHANTI YA ILALA YAENDEREA KUSHAMIRIKA KUSHIRIKI KLABU BINGWA KWA MARA YA KWANZA



viongozi na wachezaji wa timu ya ngumi ya ashanti wakiwa katika picha ya pamoja


kocha wa timu ya ashanti akitambulishwa mbele ya mashabiki

Na Addolph Bruno

UKIBAHATIKA kukaa katika kumbi mbalimbali na kushuhudia watu wakipigana ulingoni kamwe hautaacha kuingia katika kumbi hizo tena kutokana na uhondo ambao naamini utauona ukiletwa na mabondia wa mchezo huo ambao wengi hupenda kuuita masumbi.
Ni miongoni mwa michezo ambayo katika bara la Ulaya, Amerika na baadhi ya nchi za Afrika umekuwa gumzo kutokana na staili ambayo mabondia hutumia wakiwa ulingoni kiasi cha kuwafanya mashabiki kuamini kuwa huu ni mchezo hatari kumbe sivyo.
Kwa siku za hivi karibuni hapa Tanzania hususani katika jiji la Dar es Salaam zimeanzishwa klabu mbalimbali zinazofundisha mchezo huu kama Simba Boxing Club, Amana BC, Vingunguti BC, Chanika BC, Chang'ombe BC, na Gongo la Mboto BC, Kinyogori BC na zingine nyingi ambazo zimeanza kuleta manufaa ya mchezo huo ingawa zinashindwa kutokana na uendeshaji wake kuwa ghali.

Ipo klabu changa ya mchezo huu ambayo kwa miezi miwili iliyopita imekuwa gumzo katika jiji la Dar es Salaam huku wengine wakitaka kujua undani wake bila mafanikio lakini leo kupitia gazeti hili utapata uhondo wake endelea kuwa nami.
Sio nyingine ni Ashanti Boxing Club yenye makazi yake Ilala Sokoni, Dar es Salaam ambako siku za nyuma kulikuwa na timu ya Soka ya Ashanti Football Club ambayo ilipata kushiriki ligi kuu ya Vodacom kwa miaka ya nyuma na kama unavyojua imeshindwa kupeta kutokana na ugumu wa ligi mbalimbali za mpira hapa Tanzania.
Kwa waliowengi timu ya soka ya Ashanti wanatambua umhimu wake katika soka kwani iliwahi kutoa vipaji vya wanamichezo mahiri hapa kama wachezaji wa sasa wa Simba Juma Jabu, na Juma Nyosso, wengine ni Gaudence Mwaikimba, Ally Mustaphana Jabiri Azizi na Ashanti Boxing Club ni msaidizi wa Ashanti Footbal Club katika suala la ufufuaji vipaji.
Ashanti Boxing Club inayonolewa na kocha mahiri wa mchezo wa ngumi hapa nchini Rajabu 'Super D'(Mnyamwezi) ilianzishwa miezi mitatu iliyopita na wadau wa mchezo huo Nende Hamis, Robert Skauke, Emmanuel Mgaya, Jabil Mohamed, Issa Malisa, na Fadhili Ghastor ambao waliungana na kuwahamasisha vijana kuendelea kuipa heshima Wilaya ya Ilala kupitia ngumi Baada ya kushindana na mpira wa miguu.
Mwezi mmoja baada ya kuanzishwa ujio wake ulitambulidhwa kwa klabu zingine za Tanzania uliofanbyika katika ukumbi wa CCM Ilala Boma na kupokelewa kwa mafanikio makubwa na mashabiki na Hata klabu zingine zilizohudhuria kama Chanika, Gongo la Mboto na Vingunguti kutokana na umahili wa mabondia walioanza kujiunga nao.
Akizungumzia hali halisi ya klabu hiyo mwenyekiti wake Nende Hamis alisema ni klabu ambayo kama klabu zingine imejiwekea dhamira ya kuondoa mawazo ya wengi hapa nchini ya kuwa mchezo wa mpira wa miguu ndio mchezo pekee ambao unaweza kuitoa kamasomaso Tanzania kimataifa.
"Tuliamua kuungana na kuwakusanya vijana waliokuwa wakijifua wenyewe bila walimu na hata uongozi ambao ungeweza kuwapa mwongozo kama unavyofahamu kama hakuna mtu wa kuongoza kundi fulani la watu ni bure lakini pia tukiwa kama walezi wa vijana tuna dhamira mbalimbali katika klabu hii," alisema Nende.

Alisema lengo hasa la kuanzisha kwa klabu hii ni kutaka kuufanya mchezo wa ngumi urudi kama ilivyokuwa siku za nyuma na kuleta medali nyingi kama ilivyo kawaida yake mchezo huu ndio pekee ulioipa Tanzania heshima kwa kuleta medali nyingi miaka ya nyuma.
Nende alieleza kuwa timu hiyo iliamua kuungana kutokomeza umasikini kwa vijana kwa kuwapa ajira vijana wengi ambao wapo mitaani au shuleni bila kujua mwelekeo wao wa baadae na ambao wana mawazo ya kuwa wanamasumbi katika maisha yao.
Nende anasema katika harakati za kuanzisha klabu hiyo pia msimamizi wa karibu wa mchezo wa ngumi hapa Tanzania Habibu Kinyogori alihusika kwa asilimia kubwa kutoa mawazo ambapo hadi sasa ni mshauri wa karibu wa timu hiyo.

Alisema tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo wanakutana na matatizo mbalimbali lakini wao wanaendelea kuamini kuwa vikwazo ni chachu ya mafanikio katika jambo fulani ambalo binadamu analifanya na kuongeza kuwa kamwe hawatweza kuyapatia nafasi matatizo wanayokutana nayo bali watapigana mpaka waone mwisho wake hata kama wana hali duni ya kipato.

Anasema tangu kuanzishwa wamefanikiwa kuwapata mabondia kumi walioko na wasio shuleni na wana matarajio ya kuwapata zaidi ya 20 ambao wataunda timu itakayokuwa ikiwakilisha Ilala katika ngumi na kuleta upinzani wa kweli wenye nia moja ya kuendeleza ngumi hapa nchini.
Anawataja mabondia hao kuwa ni Iddi Ramadhani, Abdujerry Said, Yahaya Athumani, Juma Said, Baliki Manyota, Moris Juma, Matiku Magesa, Badiru Kassimu, Rashid Mhamila 'Ngade', Said Nayava na bondia pekee na tishio wa kike Amina Hassan.
Nende alisema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi juni wanamatarajio ya kuwa na idadi kubwa ya mabondia na kuongeza kuwa bado wanapokea vijana wenye ndoto za kuwa mabondi wakubwa kama akina Rashidi Matumla 'Snake Man' Mbana Ally, Edson Mwakyembe au Mada Maugo ambao wanaendelea kuutendea haki mchezo huu hapa nchini.

Anasema dhamira zao zitakamilika ikiwa wazazi wa mabondia hao watashirikiana nao na kuwaruhusu kujiunga na klabu hiyo na kuondokana na dhana iliyopo kwamba mchezo wa masumbwi ni hatari kwa afya ya mabondia jambo ambalo linapingwa na wadau wengi wa mchezo huu.

Alinasema kuhusu usalama wa mabondia klabu hiyo imeweka nafasi ya kwanza suala hilo kwa kusema kuwa pamoja na hali yao kuwa duni watatoa msaada kwa bondia atakayepata tatizo na kwamba katika hatua hii ya awali wapo mbioni kusaka daktari wa timu atakayekuwa akitoa huduma kwa karibu.

"Pamoja na dhamira zetu tulizojiwekea tunaona pia tutakuwa hatupo sahihi kama hatutawaomba wazazi wa mabondia kuwaruhusu kuja kujifunza kwa sababu wengi wanaamini kuwa ngumi ni hatari si kweli kwani kama ingekua hivyo mabondia maarufu kama Mike Tyson wangefia uwanjani lakini bado wapo tena wanaishi maisha mazuri kabisa na hata hapa akina Matumla wanaishi hivyo," alisema Nende.
Alisema kuwa licha ya wazazi kutoa baraka zao pia wanawaomba wadau mbalimbali wenye mapenzi na mchezo huu kuwapa mchango wao kwa njia yeyote kutokana na ukweli kwamba hapa Tanzania michezo imekuwa ikipoteza dira kwa sababu ya wahusika kuwa na kipato kidogo.
Anasema wanatoa shukrani zao za dhati kwa mdau wa ngumi mama Khalima Kaubanika kwa moyo michango yake ya kimawazo na vifaa ambavyo amekuwa akiipatia timu hiyo na kuongeza kuwa wanaimani kutokana na hilo watapata wadau wengi zaidi.

"Sisi tunaheshimu mchango wa kila mtu uwe wa mawazo au kitu chochote na kwea kuwa huu ni mwanzo tumepungukiwa vifaa vya mchezo huu kama Gumsheet, Ringboot, Joho, bukta, Grooves, ambazo ni kwa mtu wa hali ya chini ni tatizo na si hivyo tu vingine ni Vest pair, Soksi pair, na Ring bandage," anasema Nende.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa klabu hiyo Roberti Skauke anasema kuhusu walimu klabu hiyo haina tatizo kwani wanao walimu mashuhuli waliobobea kama Rajabu Mhamila 'Super D', Osker Mayuka, Juma Mawani na Baliki Manyota ambaye ni mwanamasumbi anayewasaidia walimu hao kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa awapo ulingoni.
Anasema kuwa klabu hiyo ipo mbioni kuleta walimu wengine waliobobea katika ukanda huu wa Afrika mashariki ili kuiongezea nguvu klabu hiyo na kutimiza dhamira zao walizojiwekea ikiwa ni pamoja na kuwatoa mabondia wenye hadhi ya kimataifa.
Akizungumzia suala la uongozi Skauke anasema wamejipanga vizuri kwani kila kiongozi ana sifa na nafasi aliyonayo kwa kuwa walipata kuitumikia nafasi hiyo katika sehemu zingine na kwamba hwana wasiwasi katika hilo kwani uzalendo ni kipaumbele kwa kila mmoja wao.

Anawataja viongozi wa klabu hiyo kwa ujumla kuwa ni Nende Hamisi Nende(Mwenyekiti), Robert Skauke(Katibu), Ammanuel Mgaya(Mhazini), Rajabu Mhamila(Msema Chochote wa Klabu), Jabili Mohamed (Mjumbe), Issa Malisa(Mjumbe) na Mkufunzi wao Fadhili Ghastor.

mabondia wa timu ya ashanti wakiwa katika mapambano

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...