Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 25, 2010

Mbunge Pacquiao mbino kutwangana na Mayweather

Mbunge Pacquiao mbino kutwangana na Mayweather

MANILA, Ufilipino
MANNY Pacquiao sasa anakaribia kupambana na Floyd Mayweather baada ya kukubali kufanyiwa kipimo cha damu simku 14 kabla ya pambano.
Mabondi hao kwa sasa ndiyo wakali wa ngumi duniani walikwua wapambane Machi lakini mechi yao ilifutwa.
Mechi ilifunjika kufuatia Pacquiao kukataa masharti ya Mayweather kwa kutaka apimwe damu mara mwa mara kama ilivyo katika mashindano ya olimpiki.
Kipimo hicho ni cha kuangalia kama mtu anatumu dawa za kulevya au kuongeza nguvu.
Bondia wa Ufilipino alisema hataki kupimwa damu mara wka mara kabla ya pambano kitu alichoeleza kwua ni kama hatu ya kumdhalilisha na kumfanya awe mnyonge.
Lakini kwa sasa yuko tayari kukaa meza moja na mpinzani wake na kufanya makubaliano .
Pacquiao mwenye umri wa miaka 31, alisema: "Siku 14 kabla ya mechi ni sawa kwangu, ingawa kipimo cha damu huwa hakifanyiki siku ya pambano na kiasi kidogo cha damu huchukuliwa."
Kocha wake Freddie Roach amesema kuwaPacquiao atapigana mechi moja tu na kisha kustaafu .
Pac Man karibuni amechaguliwa kuwa mbunge lakini amesisitiza kuwa anaweza akachanganya siasa na kuendela kupigana.
Pacquiao alisema: "Nitahudhuria vipindi vya bunge asubuhi na kisha jioni kwenda gym saa 10 au 11. "Nitabakia nchini wakati wa mazoezi na kisha nitasafiri kwenda Marekani wiki mbili kabla ya mechi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...