Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 23, 2010

CHOKI ATAMBA KULITEKA JIJI KATIKA UZINDUZI WA MJINI MIPANGO


ALLY CHOKI AKIIMBA

ALLI cHOKI AKIIMBA SAMBAMBA NA MWANDISHI HADIJA KALILI KATIKA MOJA YA MAONESHO YAKE

Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo 'Next Level' Ali CHoki amejigamba na kusema kuwa yupo tayari kwa utambulisho wa albamu yake ya mjini mipango ambapo amefanya mazoezi mtindo mpya wa kuingilia jukwaani
siku ya utambulisho wa albam hiyo.
Choki alitoa majigambo hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wadhamini wa utambulisho wa albamu hiyo utakaofanyika mei 28, kwaenye ukumbi wa Msasani klabu,jijini Dar es salaam ammesema kuwa anayo mitindo mingi ila tayali tayali amechagua ule atakaoingia nao na ameshaufanyia mazoezi ya kutosha akiamini utawavutia wengi watakaokuja kushughudia burudan hizo katika onesho ilo 'Napenda kusema kuwa nina mitindo 999, nimeshatumia minne, ijumaa ya utambulisho nitatambulisha wa tano ambao utakuwa babu kubwaaa,nimesha ufanyia mazoezi kwa mda mrefu na vyakutosha watu wote watakaokuwepo watafuraia kurudani hizo; alisema choki

Mwanamziki huyo alivunja rekodi ya kuingia ukumbini katika miondoko tofauti tofauti, akiwa na bendi ya afrikan star 'Twanga Pepeta' ambapo ameshawai kuingia na farasi watu wakampa jina mzee wa farasi ameshawai kuingia na tingatinga watu wakampa jina mzee wa kijiko mbali na hilo pia watu walishatunga nyimbo za kumbeza ya kwenye starehe tingatinga limefikaje

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...