Marquee
tangazo
Tuesday, May 18, 2010
WATAKAOSHIRIKI KLABU BINGWA WATAJWA
MASHINDANO ya klabu Bingwa ya mchezo wa Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam yanatarajia kuanza Mei 25 mwaka huu katika ukumbi wa DDC mwenge jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Ngumi zaq Ridhaa mkoa wa mkoa(DABA) ambao ni waratibu wake huo Remmy Ngabo alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha klabu zote za mchezo huo kutoka katika mkoa huo.
Alisema hadi sasa klabu 16 zimetibitisha kushiriki michuano hiyo ambayo itafikia kilele Mei 29 mwaka huu.
Mwenyekiti huyo alizitaja klabu zilizothibitisha kushiriki kuwa ni Magereza, ngome, JKT Mgulani, Mavituzi, Davis Corner, Ruaha Galaxy, Azimio, Sifa, Miembeni, Ndame, Polisi, Mbagala, Kariakoo, Ashanti, Uptown, na Urafiki.
"Hizi ni baadhi ya klabu zilizodhihilisha kushiriki hadio sasa lakini ni matumaini yetu kuwa tutapokea klabu maombi ya klabu zaidi ya hizi katika michuano hii mhimu,"alisema Ngabo.
Alisema klabu itakayoibuka mshindi katika mashindano hayo itakuwa imejiweka katika nafasi nzuri ya kupeperusha Bendera ta taifa katika michuano mbalimbali ikiwemo mashindano ya Majiji katika sehemu mbalimbali duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment