Na Edgar Nazar, Bagamoyo
TIMU ya soka ya Majengo star ya Magamoyo imefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya kombe la Kawambwa jimbo la Bagamoyo katika miachuno ambayo bado inaendelea katika kituo cha Magereza baada ya kufanikiwa kushinda michezo miwili ya awali.
Katibu msadizi wa Majengo star, Doto Kililo amesema kuwa huo ni mwanzo tu ambapo watakikisha kuwa wanalitwaa kombe hilo ambalo limeandaliwa na mbunge wa jimbo la Bagamoyo dkt. Shukuru Kawambwa ambaye pia ni waziri wa miundombinu.
Majengo inatarajiwa kuleta upinzani mkalia katika michuano hiyo kutokana na timu hiyo kuundawa na wachezaji nyota.
No comments:
Post a Comment