Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 11, 2010

ALEX KOBIA AIBUKA KINARA KATIKA MASHINDANO YA GOFU


Alex Kobia ameibuka kinara katika mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 37 zilizompatia ushindi.

Mashindano hayo ambayo ufayika kila mwisho wa wiki katika viwanja hivyo na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania , yalishuhudia upinzani mkubwa kutokana na washiriki kuonyeshana mchezo wenye viwango cha juu.

Kufuatia ushindi huo Kobia alizawadiwa zawadi ya mwavuli wa kisasa pamoja na seti za vyombo vya ndani kutoka Zain Tanzania .

Akiongea baada ya kupokea zawadi zake, Kobia alisema kuwa mchezo wa gofu sasa unapata umaarufu kila kukicha kutokana na idadi kubwa ya wachezaji kujitokeza kushiriki katika mashindano ya Lugalo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwisho wa wiki.

“Kama ilivyo michezo mingine mchezo wa gofu sasa unakuja juu kama ilivyo michezo mingine kwasababu kila siku wachezaji wanazidi kujitokeza na hasa vijana wadogo,” alisema Kobia.

Mbali na Kobia wachezaji wengine ambao walishinda na kuzawadiwa zawadi na Zain ni Simon Sayore, Priscus Nyoni, Moses Namuhisa, Davod Mollel na Stephania Sayore.

Klabu ya mchezo wa gofu ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam ina mkakati wa muda mrefu kwa kushirikiana na kampuni ya Zain Tanzania wenye lengo la kukuza na kuendeleza mchezo wa gofu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...