Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 16, 2010

SARA KAIS 'SHAA' AJIVUNIA MAFANIKIO KATIKA MZIKI


Shaa: “Sasa naweza kuisaidia familia”Staa wa ngoma ya Shoga, Sara Kaisi a.k.a Shaa amefunguka na kuweka wazi kwamba, hivi sasa anaweza kuisaidia familia yake wakiwemo wazazi kwa kuwa tayari ameshaanza kuchungulia mafanikio kupitia game ya muziki wa kizazi kipya.
Akiongea kupitia kituo cha redio Clouds FM cha Dar es Salaam juzi kati, Shaa alisema kwamba sanaa ya muziki ambayo aliinza tangu 2004 hivi sasa imemfanya aishi vizuri huku akiisaidia familia yake kwa mambo mbalimbali ikiwemo kuleta misosi mezani.
“Huko nyuma wakati naanza muziki sikuwa na uwezo wowote, lakini sasa naweza kuwasaidia hata wazazi wangu,” alisema Shaa ambaye hivi sasa anafanya vizuri na kupitia kazi hiyo, Shoga ambayo tayari inaonekana kupitia vituo kadhaa vya luning baada ya kufanyiwa video.http://www.abdallahmrisho.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...