Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 8, 2010

RASHIDI MATUMLA MADA MAUGO KUMALIZA UBISHA JULAI 18Mwandaji wa mpambano wa ngumi, Selemani Semunyu katikati akiwa na mabondia Rashidi Matumla (kushoto) na Mada Maugo wakati wa kutangaza mpambano wao wa kirafiki utakaofanyika julai 18


BONDIA mkongwe wa ngumi za kulipwa nchini, Rashid Matumla 'Snake Man', anatarajia kuzichapa na mpinzani wake Mada Maugo 'Junior', katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalofanyika Julai 18 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.
Akuzingumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania'TPBO', Yassin Abdalah 'Ustaadh' alisema kuwa mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni Julai 18 mwaka huu.

Alisema kuwa pambano hilo la uzito wa Middle lenye raundi 10, linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia za mabondia wote.
Abdalah alisema kuwa wameamua kuandaa pambano hilo ili kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi nchini.

Alisema kuwa pambano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Media Entertainment & Sports Promotion na linaratibiwa na TPBO.
Alisema kuwa maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na mabondia wote kuendelea na mazoezi katika kambi zao ambapo limedhaminiwa na Kampuni ya Business Times ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Business Times na Dar leo na wamiliki wa kituo cha Redio cha 100.5 Times FM na Kampuni ya Uchapishaji ya Business Printer, PSI na Konsalt..

“Tumeandaa pambano la Maugo na Matumla kwa ajili ya kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa mchezo huo, ambapo maandalizi yote yameshakamilika na tunatajia kuwa mabondia hao watatoa burudani safi” alisema Abdalah.
Alisema kuwa pia pambano hilo litatanguliwa na mapambano mbalimbali kutoka kwa mabondia chipukizi kwa ajili ya kuendeleza na kuibua vipaji vya mchezo huo.

Alisema kuwa katika pambano hilo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ambapo bondia Abdalah Mohamed atazichapa na Said Zungu katika pambano la uzito wa Light Weight la raundi nne, Fadhil Maji atapigana na Sadick Abdulaziz katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne
Wengine ni Juma Afande atazichapa na Kitandula Zuberi katika pambano la Super Bantam la raundi nne, Juma Selema atapigana na Iddy Mgodomi katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne, Anton Mathias atazitupa na Hemed Mohamed wa Ashanti boxing ilala katika pambano la Super Fly la raundi nne na Kijepa Omari atazichapa na Joseph Richard wa Ashanti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...