Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 22, 2010

ASHANTI UNITED YAANDAA DUWA YA KUMKUMBUKA MAREHEMU DITOPILE


Haji Bechina kushoto alipotembelea mayoeyi za Ashanti boxing kulia ni Iraki Hudu


Na Mwandishi wetu

KATIBU Mkuu wa klabu ya AShanti Unidet ya jijini Dar es salaam Haji Bechina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea duwa marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi Boma Ilala jijini Dar es salaam

Akizungumza na waandishi wa habari jana Bechina aliwataja watakaosomewa duwa hiyo kuwa ni pamoja aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa Mlezi wao RAjabu Mgodo, Athumani Nobi waliokuwa makatibu katika vipindi tofauti na Mzee Mwalimu Kinyogori ambaye alikuwa mwenyekiti

Bechina alisema kuwa klabu zote za mpira wa miguu zilizopo jijini DAr es salaam pamoja na wadau wa mchezo wa soka wamepewa miariko kwa kushiliki duwa hiyo itakayofanyika jumapili hii ya julay 25

Aidha klabu hiyo imepanga kuisuka upya timu ya soka ya AShanti United baada ya kupoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni

Mbali na soka AShanti pia hujishughulisha na uinuaji wa vipaji vya mchezo wa ngumi kupitia kocha Rajabu Mhamila Super D

Bechina aliongeza kuwa wanajivunia timu hiyo ya ngumi ambako mchezaji wao Joseph Richard, alimpiga kwa KO ya raundi ya pili Kijepa Omari katika pambano la utangulizi kabla ya Rashidi Matumla na Mada Maugo kwenye ukumbi wa P.T.A, Ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...