Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 23, 2010

ZANTEL HYUNDAI WAONESHA GARI YA MSHINDI WA PROMOSHENI YA DONDOKA SAUZ



Meneja mauzo wa Hyundai Antony Nyeupe (kulia) akimwonesha gari itakayoshindaniwa na wateja wa kampuni simu ya Zantel Meneja Masoko wa Zantel wiliam Mpinga Dar es salaam jana zawadi hiyo himetolewa na kampuni

HYUNDAI/ZANTEL WAZINDUWA ZAWADI KUBWA YA PROMOSHENI YA DONDOKA SAUZ
Dar es Salaam, Julai 23, 2010: Kampuni ya magari ya Hyundai wakishirikiana na kampuni ya Zantel leo wamezinduwa Zawadi kubwa itakayotolewa kwenye droo ya mwisho ya promosheni yao inayoendelea ya Dondoka Sauz. Zawadi hiyo ni gari jipya aina ya Hyundai Tucson ix35 muundo wa mwaka 2010 yenye thamani ya milioni 50 fedha za kitanzania.
Gari lipo makao makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam na linaonyeshwa bure kwa umma. Gari hili lina vikorombwezo vya hali ya juu vilivyowekwa kuhakikishia usalama. Meneja Mauzo wa Hyundai Anthothy Nyeupe akielezea vikorombwezo hivi alisema “Gari hili limetengenezwa kutoa ufahari na vikorombwezo ilivyonavyo ni kama kadi ya kuwashia gari, uwezo wa kushika breki yenyewe kwenye mteremko au mlima, breki za dharura pamoja na vioo vya pemeni kwa ajili ya usalama.”
Akielezea jinsi ya kushriki promosheni hii, Mkurugenzi Masoko wa Zantel Ikechukwu Kalu alisema “Ili kushiriki promosheni hii, mteja wa Zantel anahitaji kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno FIFA2010 kwenda namba 15726 na moja kwa moja watakuwa wameingizwa kwenye promosheni hii. Promosheni hii ni kwa ajili ya wateja wa zamani na wapya wa Zantel na kwa wale wasio wateja wa Zantel wanachotakiwa kufanya ni kununua sim kadi ya Zantel na kuanza kutuma message nyingi kujiwekea nafasi nzuri za kushinda. Zawadi kuu ya promosheni hii ni gari mpya aina ya Hyundai Tuscon ix35 muundo wa mwaka 2010.”
Droo ya mwisho ya mwisho itafanyika LIVE makao makuu ya Zantel Jumatatu tarehe 9 Agosti, 2010 na mshindi mmoja atabahatika kujishindia gari jipya aina ya Hyundai Tucson ix35 muundo wa 2010 lenye thamani ya milioni 50.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...