Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 31, 2010

STARS KUKIPIGA NA MISRI NCHINI MISRI AUGASTI 11 HUKO KOCHA WA STARS KUWASILI LEO


TAIFA STARS.

Timu ya taifa ya wanaume taifa stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya misri Augasti 11 mwaka huu nchini misri ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kushiriki fainali za kombe la DUNIA nchini BRAZIL.

Msemaji wa TFF FLORIAN KAIJAGE amesema katika harakati za kutafuta timu wakafanikiwa kupata timu ya misri.

Mchezo huo unatambulika na FIFA kwani siku hiyo ya mchezo ni siku iliyopangwa na FIFA kwa ajili ya mechi za kirafiki za FIFA.

Wakati stars ikijiandaa na mchezo huo tayari kocha wa timu ya stars JAN PAULSEN anatarajia kuwasili jumamosi usiku kuja kukinoa kikosi cha stars

NA JANE JOHN

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...