Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 19, 2010

RASHIDI MATUMLA ASTAFU NGUMI BAADA YA KUPIGWA NA MADA MAUGO JANA


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, jana aliibuka mshindi baada ya kumchapa mpinzani wake Rashid Matumla katika pambano lisilo la ubingwa la raundi kumi lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA, jijini Dar es salaam.

Katika pambano hilo la uzito wa Middle, lilikuwa na upinzani mkali ambapo Maugo alitumia nafasi alizokuwa akizipata kwa kumchapa makonde mpinzani wake katika raundi 10 walizocheza.

Baada ya pambano hilo kumalizika mwamuzi wa mchezo Ally Bakari 'Champion' alimtangaza Maugo kuwa mshindi baada ya kushinda kwa pointi 100-95, 98-98 na 96-98.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Maugo amesema kuwa ametimiza ahadi yake aliyowaahidi mashabiki wake ambapo kwa sasa anajifua kwa ajili ya kuzichapa na Fransis Cheka.

“Nimetimiza ahadi yangu niliyowaahidi mashabiki wangu hivyo kwa sasa najipanga upya kwa ajili ya kupigana na Cheka” alisema maugo.

Naye Matumla amesema kuwa amekubali matokeo katika pambano hilo hivyo kwa sasa anastaafu ngumi na kuamua kuwa kocha wa vijana ili aweze kuibua vipaji na kukuza mchezo huo.

“Nimekubali matokeo ya pambano langu na Maugo hivyo kwa sasa naachana na ngumi na ninatarajia kuwa kocha kwa ajili ya kuibua vipaji kwa vijana” alisema Matumla.

Katika mapambano ya utangulizi ya raundi nne nne, bondia Joseph Richard wa Ashanti boxingi ya Ilala Dar es salaam alimchapa Kijepa Omary kwa KO katika raundi ya pili katika pambano la uzito wa Super Fly, Mwalimu Mussa alimchapa kwa pointi mpinzani wake Masoud Mohamed katika pambano la uzito wa Super Bantam.

Mapambano mengime yalikuwa sare ambapo bondia Abdalah Mohamed alizichapa na Said Zungu katika pambano la uzito wa Light, Juma Seleman alizichapa na Iddy Mgodomi katika pambano la uzito wa Fly na Fadhil Majia alizipiga na Sadiq Abdulazizi katika pambano la uzito wa Fly.Mabondia Rashidi Matumla (kuliaa) na Mada Maugo wakichuana katika mpambano wao uliofanyika katika katika ukumbi wa PTA Dar es salaam jana Maugo alishinda kwa pointi na kumfanya matumla kutangaza kustafu ngumi matumla atangaza kuwa kocha
mashabiki wa ngumi walikuwepo kushughudia

Mabondia Josephe Richard wa AShanti (kushoto) na Kijepa OMari wakichuna katika pambano la utangulizi Richard arishinda kwa KO, ya raundi ya pili
Mabondia mada Maugo na RAshidi Matumla wakichuana

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...