Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 19, 2011

AISHA MADINDA ATAMBULISHWA KUTUA JUKWAA LA EXTRA BONGO

Na Michael Machellah, jijini Dar
MNENGUAJI mahiri wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Aisha Madinda leo ametangazwa kujiunga rasmi na bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mnenguaji huyo Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, alisema kuwa anajisikia faraja zaidi kumnasa mnenguaji huyo ikiwa ni sehemu ya kuzidi kuimarisha safu ya unenguaji kwa kuwa na watu wa sekta hiyo walio mahiri na uzoefu.

Aidha Choki, alisema kuwa baada ya kuwanasa wanenguaji mahiri wa kiume wenye uzoefu wa siku nyimgi, Super Nyamwela na wenzake, alikuwa bado anandoto za kuwa na wanenguaji wa kike wenye uzoefu kama Aisha ambaye tayari amekwisha mnasa, huku akiamini kuzidi kuimarihs kikosi chake na kujiongezea mashabiki.

Naye Aisha Madinda, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa rasmi, alisema kuwa ameamua kutua jukwaa la Extra Bongo ili kuweza kuungana na wacheza shoo wenzake wenye uzoefu ambao anaamini nao wametua jukwaa hilo kulingana na uzoefu wa wanamuziki wanaounda bendi hiyo.

“Unajua siku zote ukifanya kazi na wanamuziki wazoefu na moyo wa kufanya kazi hata wewe pia unakuwa na moyo wa kufanya kazi na kukuza kipaji zaidi na kuongeza ozoefu na hata kupiga hatua na hasa katika anga hii ya muziki wa dansi.” Alisema Aisha

Aisha tayari ameshaanza mazoezi na atatambulishwa rasmi kwa mashabiki jumatno katika onyesho lake la kwanza litakalofanyika kwenye ukumbi wa Klabu Masai Ilala jijini Dar es Salaam.

Kiongozi wa wacheza Shoo, Super Nyamwela alimkaribisha Aisha kwa mikono miwili na kusema sasa kazi imekamilika na kuwataka mashabiki na wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza ili kushuhudia mambo mapya ya mnenguaji huyo aliyotuanayo katika bendi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...