Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 28, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGA MWILI WA MAREHEMU PROFESA MUSHI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, na ndugu jamaa na marafiki, wakiwa katika shughuli za mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya marehemu.
Mtoto wa marehemu Profesa Samuel Mushi, Susan Mzee, akitoa shukrani kwa niaba ya familia ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...