Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 29, 2011

NANI KUIBUKA MSHINDI WA MISS ILALA LEO

REDDS MISS ILALA KUNYAKUA MILIONI 1.500.000 IJUMAA

Shindano la kumtafuta Mrembo wa Kanda ya Ilala linafikia kilele ijumaa wakati Walimbwende kumi na saba watakapo panda jukwaani kumenyana wakishindania Taji la Redds Miss Ilala ikiwa ni kwenye mchakato wa kuelekea kumpata Mrembo wa Tanzania.
Kila kitu kiko tayari kwa ajili ya Mashindano haya ambayo yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. Warembo wamekamilika, maandalizi yote yako sawa sawa ikiwa ni kubadilisha kabisa maandhali ya viwanja vya Mnazi mmoja kutoka katika hali ya kuwa vya mikutano ya hadhara na kuwa katika hali ya viwanja vya starehe na burudani.
Michoro ya jinsi viwanja vitavyo onekana imetokana na Taman min Indonesia park iliyoko katika jiji la Jakarta na tunategemea kuwa kila atakayefika mahala pale atapata burdani tosha na kumfanya kuweka shindano la mrembo wa Ilala mwaka huu kuwa kumbukumbu kwake.
Bendi ya African Stars Twanga Pepeta itaanza kutumbuiza kuanzia saa moja kamili jioni na kutoa burdani kwa watu watakaokuwa wanaingia uwanjani hapo. Burdani pia itaporomoshwa na Mwanamuziki wa ngoma za asili Wanne Star na Warembo walioingia fainali katika Shindano la Vipaji.
Zawadi zitakazo tolewa kwa warembo ni kama ifuatavyo:
1. Redds Miss Ilala atapata Tshs 1,500,000/=
2. First Runner Up atapata Tshs 1,000,000/=
3. Second Runner Up atapata Tshs 850,000/=
Hawa watapata pia tiketi ya kuwakilisha Miss Ilala katika shindano la Vodacom Miss Tanzania.
4. Third Runner Up atapata Tshs, 500,000/=
5. Fourth Runner Up atapata Tshs. 500,000/=
6. Kifuta Jasho kila mmoja atapata Tshs 200,000/=

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...