Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 3, 2011

ANDY COLE ATUA BONGO NA KUSEMA MCHEZAJI BORA DUNIANI ATOKE TANZANIA

KIKOSI CHA U-17
COLE AKISALIMIANA NA MKURUGENZI MSAIDIZI WA IDAYA YA MAENDELEO NA MICHEZO, JULIANA YASODA
NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO DK.FENELA MUKANGARA AKIMKABIDHI JEZI COLE AM,BAZO WATATUMIA VIJANA HAO.

COLE AKIZUNGUMZA MACHACHE

Na Dina Ismail
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Manchester United Andrew ‘Andy’ Cole ametua leo nchini na kuzindua programu maalum yenye lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wenye mri chini ya miaka 17 barani Afrika ijulikanayo kama ‘Airtel Rising Stars’.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika katika sekondari ya Makongo, Cole alisema anaamini vijana watakaopata nafasi ya kushiriki katika progamu hiyo kama watafanya juhudu watafanikiwa kupata nafasi ya kuzichezea timu kubwa duniani.
“Nafurahi kufika Tanzania na kuhamasisha vijana wa huku kushiriki katika mpango huu, …ingawa kuna joto lakini haijalishi, naamini kama vijana watajibidiisha watafanikiwa, pia naamini mchezaji bora wa Afrika atatoka Tanzania,”Alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...