Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 2, 2011

Wanyange Redds Miss Temeke kutembelea Vodacom

Miss Temeke 2010 ambaye ndiye Miss Tanzania 2010
Genevieve Emmanuel
 WANYANGE wanaowania taji la Redds Miss Temeke, kesho watatembelea makao makuu ya wadahamini wakuu wa Miss Tanzania, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya kumsaka mrithi wa Geneveive Mpangala.

Kambi ya Redds Miss Temeke iliyoanza rasmi mwanzoni mwa wiki hii, ipo chini ya wakufunzi Carlo Zayumba na Anna Daud sanjari na Dickson Detram kwa upande wa shoo, katika ziara yao ya leo(kesho Ijumaa) mbali ya kuelezwa kazi za kampuni hiyo yenye mafanikio makubwa kati ya makampuni ya simu za mkononi, pia wataelezwa nafasi ya Vodacom katika kuayafanikisha mashindano hayo.


Taji la Miss Tanzania linashilikiliwa na Miss Temeke 2010,Geneveive ambaye pia ni Miss Tanzania kupitia kanda hiyo, alikuwa mshindi wa Redds Miss Temeke mwaka jana alipopata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania sanjari na washindi wengine wawili, Anna Daudi na Britney Urassa.

Wanyange wa mwaka huu ni pamoja na Cynthia Kimasha, Elizabeth Boniface, Eunice Mbuya, Husna Twalib, Irene Jackson, Joyce Maweda, Lucia John, Mwajuma Juma, Naifat Ally, Naomi Ngonya, Prisca Stephen, Sasha Seti, Sara Said, Sara Paul na Victoria Mtega.
Mbali ya Geneveive, warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Tanzania kupitia Temeke ni pamoja na Happiness Magesse 'Millen' (2001) na Sylvia Bahame mwaka 2003. Pia warembo Jokate Mwegelo aliwahi kutwaa taji la ubalozi wa Redds huku mwaka 2009, Sia Ndaskoy alishinda taji la ubalozi wa Utalii.

Mashindano ya Miss Temeke yalianza mwaka 1996 ambapo mshindi alikuwa mwandaaji wa Miss Shinyanga, Asela Magaka. Warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Temeke ni pamoja na Khamisa Miriam Odemba(19997), Khamisa Ahmed(1998) na Ediltrda Kalikawe(1999).

Wengina ni Irene Kiwia(2000) na Happiness Magese 'Millen'(2001).Regina Mosha (2002), Slyvia Bahame(20030, Cecylia Assey(2004), Seba Agrey(2005), Jokate Mwegelo(2006), Queen David(2007), Angela Lubala(2008), Sia Ndaskoy(2009) na Genevive Mpangala anayeshikilia taji hilo.

Safari ya kuelekea Vodacom Miss Tanzania ambapo mshindi wa mwaka huu atakwenda London nchini Uingereza katika mashindano yatakayofanyika Novemba 6, yatakayoambatana na sherehe za kutimiza miaka 60 ya mashindano ya urembo ya Dunia ambayo yalianza mwaka 1951.

Mbali ya kampuni ya bia nchini TBL kuwa wadhamini wakuu kupitia kinywaji chake cha Redds Original, wadhamini waliokwisha thibitsha hadi sasa ni Vodacom Tanzania ambao pia ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, gazeti la Jambo Leo na saluni ya kisasa iliyopo katikati ya jiji ya Sally Salon.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...