Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 10, 2011

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JIJINI MBEYA LAPAGAWISHA MASHABIKI, YAANI WANAJISIKIA MAJOTROO TU


Mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta tayari umepamba moto katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, ambapo wasanii mbalimbali tayari wamepanda jukwaani na kufanya mambo makubwa katika jukwaa la Serengeti Fiesta jioni hii.
Juma Nature kulia akiimba kwa pamoja na wasanii wa lililokuwa kundi lao zamani TMK Family Katika tamasha hilo lililomalizika muda mfupi uliopita katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, katikati ni Dj Snocks na kushoto ni Dollo.
Watu wengi wanaonekana kuwa wenye furaha na wanaojisikia Majotroo kwelikweli katika tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL, kwani wamekuwa na mzuka wa kweli wakati wotw wa tamasha hilo.
Roma akiwakilisha katika tamasha hilo.
Kundi Tiptop Connection wakishabulia jukwaa katika tamasha la Serengeti Fiesta jijini Mbeya.
Mashabiki wa muziki wa mjini Mbeya wakiwa wamepata Majotroo kama unavyowaona wakiwa wanacheza kwa staili tofauti ili mradi kujipa raha.
, Hapa anaonekana mwimbaji wa muziki wa Hiphop Prof. Jay akiimba nyimbo zake, kama vilee piga makofi katika tamasha hilo llililovutia watu wengi.
Profesa Jay akiimba na mmoja wa mashabiki wake aliyemuita jukwaani ili kumpa tafu katika moja ya nyimbo zake.
Mashabiki wakinyanyua mikono yao juu kuashiria kukubali muziki uliokuwa ukiporomoshwa na wasanii wa tamasha la Serengeti Fiesta jijini Mbeya jioni hii.
picha na mtandao wa http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...