Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 21, 2011

GRAND MALT YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO VYA SH. M. 10 KWA TIMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI

Waziri wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad (kushoto) akipokea jezi kutoka kwa Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam, kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar itakayopambana na timu ya Klabu ya Wazee ya Arusha Septemba 8, mwaka huu. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Baraza, Mbarouk Mussa. Kampuni hiyo ya Grand Malt imetoa vifaa hivyo vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10. Picha na Martine Kabemba
Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad akionyesha viatu walivyokabidhiwa.
Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad (wa pili kushoto), Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Mbarouk Mussa (kushoto), pamoja na Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam (kulia) wakigonganisha vinywaji vyao vya kopo za kinywaji hicho wakati wa hafla ya timu hiyo kukabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10, mjini Zanzibar.

Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad akizungumza ikiwa ni sehemu ya kushukuru kinywaji cha Grand Malt kwa kuruhusiwa kudhamini michezo na shughuli mbalimbali katika Visiwa vya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...