Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 16, 2011

ILALA WAPATA SAPOTI YA MAJI KWA AJILI YA MAPAMBANO YA JUMAPILI JULAI 17
MCHAKATO wa Kuendeleza mchezo wa ngumi za Ridhaa Katika Mkoa wa
Kimichezo wa ILALA, unatarajiwa kuingia katika hatua nyingine Julai 17 kati ya klabu za ngumi ya Amana, Matimbwa,Ashanti,Bigrayt na klabu nyingine

Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa
Panandi Panandi uliopo bungoni Wilaya ya ILala ambapo mabondia wanne
kutoka katika kila klabu, watachapana makonde.

Mabondia wa Amana watakaopanda siku hiyo ni IBrahimu Class Kg.64,
Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48.
Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na MOhamedi Matimbwa Kg 64, MOhamedi
Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na MOhamedi Kumbilambali Kg 48 na Klabu ya Ashanti ni Uwesu Manyota,Ramadhani Kimangale,Mark Edson

Akizungumza Dar es Salaam leo Mratibu wa mapambano hayo ambae pia ni
kocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, Rajabu
Mhamila Super D, Alisema mpango huo utaendelea mpaka wahakikishe
wamefanikiwa kuibua vibaji na kuviendeleza

Alisema tangu waanze mpango wa kuandaa mapambano mkohani humo
wamefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo mkoani humo na kuwataka
wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili upate kuendelea
ambapo Super D alitoa mfano wa vitu wanavyoviitaji ikiwemo posho za
nauli kwa wachezaji vifaa vya kuwatia moyo na zawadi mbalimbali kwa
mabondia

Super D aliwashukulu wadau waliojitolea katoni 15 za maji kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo yatakayofanyika jumapili ya Julai 17 aliwataja waliosaidia kuwa Mohamed Sadiq 'Muddy Kala' na Mwanamama Halima Kaubanika aliyejitolea maji kwa wachezaji wote watakaocheza kwa siku hiyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...