Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 14, 2011

ANNA LUKINDO ATINGISHA KWA MITINDO YA MAVAZI JIJINI LONDON


Jestina akionyesha baadhi ya mitindo ya mavazi yaliyobuniwa na Mtanzania Anna Lukindo.

SALAM,
Mtanzania mbunifu wa mitindo ya nguo Anna Lukindo ametikisa ulimwengu wa fashion jijini london wikiendi iliopita. Anna alionyesha mavazi aliyobuni kwenye maonyesho ya La Geneve North Event, yaliyofanyika London siku ya ijumaa tarehe 8.7.11 Ubunifu wa Ann ulipokelewa kwa vifijo na nderemo kwani ulikuwa ndio uliotia fora.
Kulikuwa na wabunifu wengine kumi lakini Anna ndio alikuwa mwafrika na Mtanzania pekee ambaye Mavazi yake yalikubalika na kupendwa na watu wengi zaidi.
Mojawapo ya wageni na wadau mbalimbali walijjitokeza kumpa sapoti Anna ni Mh Balozi wetu Peter Kallaghe na Mama Balozi, Naibu Balozi Chabaka Kilumanga pamoja na watanzania wengine.
Kwa niaba ya URBAN PULSE Tunapenda Kumpongeza Dada yetu Anna Na Kumtakia kila la kheri pamoja na Mafaniko Mema.
Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea
Anna LuksPr/Media:Pauladpope@yahoo.co.ukWeb:www.annaluks.comTwitter:@AnnaLukindo
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE
urbanpulsecreative@googlemail.com
Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe akiwa na baadhi ya Staff wa Ofisi ya Ubalozi ambao walijitokeza katika kumpa sapoti Mtanzania.

Onyesho la mitindo yaa mbavazi likiendelea.

Model akiwa mzigoni.

Model Tina,Anna,Tammy,Zulfa na Rafiki Ann.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...