Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 1, 2011

NAPE ATEMBELEA 'NEWSROOM' ZA MWANANCHI NA GLOBAL PUBLISHERS

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye(kulia) akikumbatiana kwa fraha na Mhariri Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Daniel Msacky,alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd, Tabata, Dar es Salaam, 29/6/2011. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Sixtus Mapunda.


Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga, Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga.

Waandishi wa habari wakiwa kazini katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd.

Mhariri wa Habari wa Mwananchi, yahya Charahani akiwa kazini.


Mwandishi wa habari mkongwe wa Lauden Mwambona wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, akifurahi Nape alipoingia chumba cha habari cha magazeti ya kampuni hiyo.


Nape akionyeshwa maandalizi ya gazeti la Mwananchi katika hatua ya mwisho kabla ya kwenda kuchapwa mtamboni. Anayempa maelezo ni Makunga.


Meneja uzalishaji katika mtambo wa uchapaji magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Sameer Aher akimweleza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye sehemu ya mtambo huo inavyofanya kazi.Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa MCL Theophil Makunga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...