Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 27, 2011

SUPER NYAMWELA KUTOKA NA RAP MPYA YA 'NASAKA MAHELA' NDANI YA EXTRA BONGO

Mnenguaji mahiri wa bendi ya Extra Bongo ‘Super Nyamwela’ yupo mbioni kuipua rap yake mpya inayokwenda kwa jina la Nasaka Mahela, atakayoitumia katika wimbo mpya uliotungwa na Roggat Hegga Katapila uitwao Ufisadi wa Mapenzi.

Akizungumza na Mtandao huu wa Sufianimafoto, Nyamwela alisema kuwa, wimbo huo umerekodiwa katika Studia ya Sofia Records utakaotoka sambamba na video yake ambayo pia itarekodiwa katika studio hiyo.

Aidha Nyamwela alisema kuwa pia katika albam mpya ijayo ya bendi hiyo atakuwa na kibao chake alichotunga mara tu baada ya kutua katika bendi hiyo akitokea African Stars Twanga Pepeta, ambao bado unaendelea kufanyiwa mazoezi na wanamuziki wa bendi hiyo.

Bendi hiyo ya Extra Bongo iliyo chini ya Mkurugenzi wake Ally Choki, ipo katika maandalizi ya albam yao mpya inayotarajia kukamilika hivi karibuni.
Mnenguaji Super Nyamwela ambaye pia ni kiongozi wa Safu ya wanenguaji wa bendii ya Extra Bongo (kulia) akishambulia jukwaa pamoja na wanenguaji wenzake katika moja ya onyesho lao lililofanyika hivi karibuni
http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...