Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 21, 2011

VIDEO YA MIAKA 50 YAZINDULIWA RASMI
Mwenyekiti wa chama cha Wanamuziki,Tanzania Flava Unit akizungumza mapema leo kuhusiana na uzinduzi wa video ya miaka 50 ya uhuru wa sanaa ya Muziki,video hiyo imefanywa na kampuni ya Visual Lab,ina jumla ya dakika zisizozidi nne ili watazamaji wasichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36. Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Msemaji Mkuu wa Tanzania Flava Unit,Mkubwa Fella akiwatambulisha viongozi waandamini wa chama hicho,mapema leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.kushoto kabisa ni Mjumbe wa chama hicho Keisha.
Msemaji mkuuu wa chama cha Tanzania Flava Unit,Mkubwa Said Fella akiendelea kuwatambulisha viongozi wa chama hicho,wa kwanza kulia ni Mjumbe Banana Zorro,Prodyuza wa Chama hicho Lamar Niekamp kutoka Fish Crub,Katibu Kalla Pina na anaefuata kushoto ni Khalid Mohamed ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa Tanzania Flava Unit.
Baadhi ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengeine wakiangalia 'DEMO' ya video hiyo iliyozinduliwa leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Ndugu zangu habari za mchana,

Nachukua fursa hii kuwakaribisha katika uzinduzi wa video ya wasanii inayohusiana na sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, hii ni sehemu yetu na sisi ya kusherehekea kama vijana tukionesha kuguswa kwetu na hili, na wakati huo huo tukijaribu kuonesha mchango wetu kama vijana kwa serikali yetu ambayo kwa njia moja ama nyingine inahitaji shukrani, kwani ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.

Tuna uhuru, tuna amani na mambo yanaenda ingawa matatizo ya hapa na pale yapo, lakini tumeangalia upande mzuri zaidi na tumeona kabisa huu ndio muda muafaka wa kukumbushana pale tuilipojikwaa, ili tupate kwernda kwa mwendo mzuri.

Katika miaka hii 50 ya Uhuru sanaa ya muziki ni moja kati ya sekta ambazo zimeleta ajira kwa vijana. Unaweza kuona jinsi wasanii mbali mbali walivyojikwamua kupitia muziki, mifano hai imo hata humu ndani, watu wanaendesha magari, watu wanaishi kwenye nyumba nzuri na wana miradi yao kupitia muziki huu wa kizazi kipya.

Si vibaya basi kwa kile kidogo unachokipata kukitolea shukrani, kuonesha kwamba unakithamini, sisi twajivunia miaka 50 ya uhuru na tunahisi kwamba tuna kila haja ya kusherehekea.

Sisi kama Tanzania Flava Unit, vijana ambao tuko katika sekta ya muziki tuliojikusanya kwa lengo la kuufikisha muziki wetu katika eneo jingine kimaudhui tumepania kufanya matamasha mengi tu nchi nzima, katika kusherehekea hili na yote haya yatakuwa ya wazi, na tutakuwa tukitoa burudani kwa watanzania, tukisherehekea nao pamoja miaka hii 50.

Kwa fikra zetu hii ni muhimu, kuna wakati mtanzania anahitaji burudani na hawezi kuingia sehemu kulipa wala hawezi kufika mahali mbali kabisa akaniona ama mimi, au Chegge ama temba, kwa nini tusimfikie na kumpa burudani?
Hilo lilikuwa wazo la kwanza.

Lakini jingine ni kwamba kuna wakati mtanzania anahitaji kuburudika, kashafikiria sana mfumuko wa bei, kafikiria sana suala la umeme ambalo linatusumbua wengi na kafikiria sana ugumu wa maisha, na mwisho wa siku akitoka nje katika uwanja wa karibu anapata burudani angalau anachangamsha ubongo wake na kuanza kujua kesho atakabiliana vipi na ugumu huu wa maisha ambao kila kukicha tunajitahidi kuhakikisha kwamba tufike sehemu, ila mtu apate unafuu.
Tuko katika hatua za mwisho kabisa kupata udhamini wa kufanya matamasha haya, na tukiwa tayari tutawafahamisha.

Video hii imefanywa na kampuni ya Visual Lab, ina jumla ya Dakika zisizozidi nne ili msichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36.

Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Hili ndio kubwa kwa leo kaka na dada zangu iwapo kuna la ziada tutaambiana!

Hamis Mwinjuma.
Mkurugenzi
Tanzania Flava Unit

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...