Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 29, 2011

LUDACRIS: NINAZO NYIMBO ZA KUTOSHA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WANGU KATIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JUMAMOSI


Mwanamuziki Ludacris kutoka nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika asubuhi hii kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dare es salaam, Ludacris alikuwa akizungumzia onyesho lake atakalolifanya kesho, katika tamasha la Mwendelezo wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwabja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, katika picha kulia ni Mkurugenzi wa radio Clouds Ruge Mutahaba. Ludacris amesema anazo albam saba hivyo katika albam hizo anatarajia kutoa burudani ya kutosha ili kukonga mioyo ya mashabiki wa wa muziki wake nchini Tanzania
Mwanamuziki Ludacris wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Ruge Mutahaba mkurugenzi Clouds kushoto ni Caroline Ndungu, aliyekuwa mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers na Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo.
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungamza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati alipozunguzia tamasha la Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, katikati ni Mwanamuziki Ludacris na mwisho ni Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba.
http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...