Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 23, 2011

EXTRA BONGO,MKESHA WA X-MASS NDANI YA MEEDA


Na Michael Machellah

MKURUGENZI wa Bendi ya Extra Bongo,Ally Chocky aahidi kufatoa burudani ya pekee katika Mkesha wa Chrismas,jumamosi katika Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Chocky amesema katika shoo hiyo patakuwa na ushindani wa pekee kati ya wanamuziki na wacheza shoo ambapo Mkurugenzi mwenyewe,Ally Chocky atapanda jukwaani kuchuana na Mwalimu wa walimu,Banza Stone kwa kutoa shoo na baaada ya hapo watahamia kwa wacheza shoo wa kike ambapo Mkongwe wa Dance, Aisha Mbegu atachuana na Otilia Boniphace (Kandoro).

Murugenzi alisema, katika onyesho hilo la Mkesha wa Chrismass wataporomosha nyimbo mpya ambazo wanarekodi katika kipindi hiki pamoja na kukumbushia nyimbo zilizotamba enzi hizo kama Fadhira kwa wazazi ya Rogath hega Katapila,Mwaka wa tabu na zinginezo

Wapenzi na mashabiki wa Bendi ya Extra Bongo wajitokeze kwa wingi kushuhudia mambo mapya ya Bendi yao na pia kukaa pamoja katika kukaribidsha kuzaliwa kwa Yesu Kristo yaani Chrismas

Bendi hiyo jumapili itaendelea na shoo katika Ukumbi wa Magereza yaani sikukuu yenyewe na juma lijalo itarejea katika ratiba yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...