Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 15, 2011

WEMA VS DIAMOND & JOKATENa Imelda Mtema

KISHINDO cha Jokate Mwegelo ni kizito, kimeingia ndani ya uhusiano wa brazameni, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu kisha kuwafanya wawili hao kila mmoja kushika hamsini zake.
Wema, amefunga virago, ameondoka nyumbani kwa Diamond, Sinza Madukani, Dar es Salaam kwa mtindo wa “wanakwenu kwa heri, nimechoka masimango, narudi nyumbani kwetu leo.”
Madai ‘yanahiti pointi’ kuwa Diamond na Jokate wapo kwenye penzi jipya lenye nguvu, Wema ameligundua hilo, ameona ni maji marefu, kwa hiyo amejiweka pembeni kuepuka…
Na Imelda Mtema
KISHINDO cha Jokate Mwegelo ni kizito, kimeingia ndani ya uhusiano wa brazameni, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu kisha kuwafanya wawili hao kila mmoja kushika hamsini zake.
Wema, amefunga virago, ameondoka nyumbani kwa Diamond, Sinza Madukani, Dar es Salaam kwa mtindo wa “wanakwenu kwa heri, nimechoka masimango, narudi nyumbani kwetu leo.”
Madai ‘yanahiti pointi’ kuwa Diamond na Jokate wapo kwenye penzi jipya lenye nguvu, Wema ameligundua hilo, ameona ni maji marefu, kwa hiyo amejiweka pembeni kuepuka msongamano.
Inazidi kudaiwa kwamba Wema alijaribu kumfanya Diamond atulie lakini ikashindikana, ilipodhihirika Jokate ameshika mpini, alianza kupata mateso ya moyo na hisia kwa jinsi alivyofanywa ‘spea tairi’. Madai ‘yanahiti’ pia kwamba Wema alithibitisha kuwa Diamond na Jokate wanamchezea ‘ukuti ukuti’ baada ya kuwafumania wakiwa ‘vere klozi’ kimahaba kwenye Hoteli ya Picolo, Masaki, Dar es Salaam. Hata hivyo, inadaiwa kuwa Wema alipowakuta Diamond na Jokate, hakuangusha varangati kama mmiliki, badala yake alinywea utadhani yeye ndiye mwizi kisha akawaambia: “Samahanini sana kwa kuwaingilia kwenye starehe zenu.”

VITA YA TANGU ENZI
Wema na Jokate, walipambana kwenye vita ya kuwania Taji la Miss Tanzania mwaka 2006 lakini safari hii wanapambana kwa ajili ya penzi la mwanaume. Mwaka 2006, Wema aliibuka kidedea kwa kuchukua taji, wakati Jokate alishika nafasi ya pili, safari hii inaonekana kibao kimegeuka, kwani Miss Tanzania huyo bila kulazimishwa, mwenyewe kainua mikono na kutimka. NENO LA WEMA Wema akizungumza na paparazi wetu baada ya kurejea nyumbani kwao, Sinza, Mori, Dar es Salaam, alisema kuwa ameondoka kwa Diamond baada ya kujiridhisha kwa ushahidi wa kina kwamba anatoka na Jokate. Mrembo huyo alisema, anaumia kwa sababu aliamua kutulia na Diamond kwa mapenzi yote na uaminifu, kumbe mwenzake hakuwa na utulivu.
“Unajua watu wengi wanajua mimi situlii na mwanaume mmoja kitu ambacho nakipinga kabisa, kwa maana kuna wakati navumilia ninayofanyiwa na wanaume lakini inashindikana,” alisema Wema. Staa huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kujua uhusiano unaoendelea kati ya Diamond na Jokate, aliamua kujifanya mjinga ili mchumba wake huyo ajirekebishe lakini bado akawa anasikia habari hizo. “Nimeona bora nirudi nyumbani kwetu nikapumzike kwanza, kwa maana nyumbani kwetu sijafukuzwa wala hakuna shida yoyote,” alisema Wema.
JOKATE NAYE
Jokate alipozungumza na ripota wetu, alisema kuwa hana bifu na Wema kwa sababu hajawahi kumfanyia ubaya wowote. “Sijatembea na Diamond, nilikuwa karibu naye kikazi. Wimbo mpya wa Diamond unaoitwa Mawazo, video yake na mimi nimecheza. “Ni kweli kuna maeneo kadhaa nilikuwa naambatana na Diamond lakini siyo kimapenzi. Nilikuwa naye kikazi, siyo kimapenzi hata kidogo,” alisema Jokate.
WOLPER TEH TEH TEHEE!
Kabla ya Jokate kuingilia kati, Wema alikuwa na bifu na staa mwenzake wa filamu, Jacqueline Wolper kwamba ndiye anamuingilia katika mapenzi yake na Diamond. Bifu hilo, lilikuwa kubwa kutokana na tuhuma kuwa Diamond alianza ‘kukong’ota’ na Wolper kabla hajatua kwa Wema. Akizungumza na ripota wetu, Shakoor Jongo juzi (Jumatatu), Wolper alisema, ni furaha kwake kubainika kwamba anayemchukua Diamond ni mtu mwingine. “Mungu Mkubwa, nilikuwa naonekana mimi ndiye tatizo, kumbe adui ni mwingine kabisa, teh, teh, teheeee!” alisema Wolper.

9 comments:

 1. poa kwa jokate coz ni mkali zaidi yao

  ReplyDelete
 2. HUYU WOLPER NI MNAFIKI SNA ANAONEKANA

  ReplyDelete
 3. Diamond hana ujanja wakutoka na Jokate hiyo itakua ni issue ya kikaz tu na si mapenzi.

  ReplyDelete
 4. hakuna mwanamke mkali/mjanja mbele ya hela wanawake wa kibongo wengi wao hasa wasanii wanaangalia mkwanja tu so jocate hachomoi kwa diamond

  ReplyDelete
 5. wema congratulations from canada, hebu tulia nawe utapata bwana wa maana achana na hawa viruka njia wanaume with no class.

  ReplyDelete
 6. wewe wema u seem to be someone from a classy family, how did u get mixed up with watoto wa mtaani? i want u to look for a film called "love brewed in an african pot" then u will understand why am asking u such a question. u cannot change leopard's spots. god bless u into finding a better man and raise a good family the way your parents did. once beaten twice shy pls don't manga manga with people of no fixed abode / love auntie cheupe in canada

  ReplyDelete
 7. the more i read about diamond and jokate the more i get disgusted with the two. honestly, hivi wewe wema what were u thinking when u fell in love with diamond? what did u see in him? hana sura, hana kisomo wala hana bongo, any way it's never too late for you dear girl, wake up and take your time to find a new lover achana na hawa vijana limbukeni jua kali. bravo to your mom and family who are always there for u / luv, from iceland

  ReplyDelete
 8. mshamba ni mshamba, wema don't waste your breath entertaining upuuzi wa diamond and jokate / these two deserve each other / acha wakunje miguu wale pilau na choroko jamvini. western world think highly of u girl / greetings from reykjavik

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...