Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 20, 2011

WAZAMBIA KUICHEZESHA TWIGA STARS UGENINI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Zambia kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia.
Mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 13, 14 na 15 mwakani. Mwamuzi ni Gladys Lengwe wakati waamuzi wasaidizi ni Patience Mumba na Mercy Zulu.
Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Bookanang Lekgowe kutoka Botswana wakati kamishna wa mechi hiyo kutoka Afrika Kusini atakuwa Smith Hilton Fran.
Mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars inayofundishwa na kocha Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Nasra Mohamed imeanza rasmi mazoezi jana (Desemba 19 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...