Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 31, 2011

Floyd Mayweather, Jr.; bondia anayetikisa katika masumbwi


Floyd Mayweather, Jr.; bondia anayetikisa katika masumbwi
*Ameshinda mapambano 26 kwa Ko

KWA mabondia wengi, wanapopanda ulingoni huhitaji ushindi mzuri, ushindi ambao hautakuwa na utata katika maamuzi kwa wahusika wote wawili.

Marekani ni moja ya nchi zenye mabondia wengi wazuri duniani, ambao wamefanya vizuri katika mapambano mbalimbali yakiwemo makubwa ya mikana mbalimbali.

Floyd Joy Mayweather (Jr), ni mmoja wa mabondai waliofanya vizuri nchini Marekani na kuweka historia katika mchezo huo wa kibabe.

Bondia huyo alizaliwa Februari 24, 1977, ni bondia wa ngumi za kulipwa wa kimataifa wa Marekani, He is a five-division world champion, alishinda mataji mara saba, likiwemo la ubingwa wa lineal katika uzito wa aina tatu.

Alitwaa tuzo mara mbili ya mwaka, ikiwemo ubingwa mwaka 1998 na 2007, pia tuzo ya waandishi wa habari za ngumi za kulipwa Marekani (BWAA), bondia bora mwaka 2007. Ni bondia ambaye hajawahi kupigwa.

Kwa sasa, Mayweather anashikilia ubingwa wa WBC uzito wa welter.Ngumi ni sehemu ya maisha yake, Mayweather ambaye alianza akiwa mdogo. Wakati watoto wengine wakijiingiza kwenye mchezo wa baseballs au soka, alikuwa akijifunza kurusha ngumi na kukwepa.

Bondia huyo alikuwa ameiweka pembeni michezo mingine na kuzingatia zaidi ngumi pekee. "nadhani, bibi yangu alikuwa wa kwanza kukiona kipaji changu," alisema Mayweather, huku akitabasamu. "Wakati nikiwa kijana, nilimweleza, 'Nadhani utapata kazi.' alisema, 'Hapana, wewe zingatia ngumi.' "

"Wakati nikiwa na miaka kati ya nane au tisa, niliishi na mama katika mji wa New Jersey na mama, tukiwa saba katika chumba kimoja, wakati mwingine tulikosa umeme", alisema Mayweather. "Wakati wengine wakiniona nilivyo, hawajui nilikotokea wakati sikuwa na kitu."

Mayweather alizaliwa mjini Grand Rapids, Mich, katika familia ya mabondia. Baba yake, Floyd Mayweather Sr. alikuwa bondia mkongwe wa uzito wa welter aliyekuwa mpinzani wa Sugar Ray Leonard, mjomba wake Jeff Mayweather na Roger Mayweather, walikuwa mabondia wazuri, wakati Roger ni mkufunzi wa Floyd, aliyeshinda ubingwa wa ngumi mara mbili.

Mayweather limetokana na jina la mwisho la mama yake, lakini jina lake la mwisho lilibadilika na kuwa, Mayweather muda mfupi baada ya hapo. Baba yake Mayweather, Floyd Sr., alikuwa upande wa kuuza madawa.

Ilikuwa siyo kitu cha ajabu kwa Floyd mtoto kurudi nyumbani na kujidunga sindano ya madawa ya kulevya, wakati mama yake pia alikuwa ameathiriwa na madawa hayo, huku shangazi yake alifariki kwa ugonjwa wa ukimwi kwasababu ya kutumia madawa ya kulevya.

Wakati wote, baba yake alikuwa akimpeleka gym kwa ajili ya mazoezi ya ngumi, kwa mujibu wa Mayweather. "Sikumbi kila alipokuwa akinichukua au kufanya chochote ama baba anachokifanya kwa mtoto wake, kwenye hifadhi au filamu au kula askrimu," alisema. "wakati wote alikuwa akisema anampenda mtoto wake wa kike.

Floyd Sr. alisema hakuwahi kumweleza mapema uhusiano wake mapema. "Ingawa baba yake alijihusisha na kuuza madawa, sikuweza kumhusisha mwanangu," alisema Floyd Sr. . "Madawa niliyokuwa nauza ilikuwa sehemu ya maisha. Walikuwa na chakula cha kutosha. Walikuwa na mavazi mazurina nilikuwa nikiwa fedha. Kila mtu atakueleza kuwa, nilikuwa nikiwajali watoto wangu."

Mayweather ana rekodi ya kushinda mapambano 84–6, katika ngumi za ridhaa, na kutwaa tuzo ya dhahabu mwaka 1993, 1994 na 1996.

Kwa ushupavu wake, alipewa jina la utani "Pretty Boy" na marafiki zake wa ngumi za ridhaa, kwasababu alikuwa makjovu machache kutokana na kulinda na wapinzani wake wakati wa mapambano.

Uwezo wake huo ulitokana na mbinu alizokuwa akifundishwa na baba yake na mjomba wake Roger, ambapo katika michuano ya olimpiki ya mwaka 1996 iliyofanyika mjini Atlanta, Mayweather alitwaa medali ya shaba, baada ya kutinga hatua ya nusu fainali katika uzito wa feather kg 57.

Katika mapambano ya ufunguzi, Mayweather aliongoza kwa pointi 10–1, dhidi ya Bakhtiyar Tileganov wa Kazakhstan, kabla ya kushinda mzunguko wa pili kwa mwamuzi kusimamisha pambano.

katika mzunguko wa pili, Mayweather alimzima Artur Gevorgyan wa Armenia kwa pointi16–3. Katika hatua ya robo fainali , bondia huyo mwenye miaka 19, Mayweather, alipigwa na bondia mwenye miaka 22, Lorenzo Aragon wa Cuba kwa pointi 12–11, na kuwa bondia wa kwanza wa marekani kuchapwa na biondia kutoka Cuba katika kipindi cha miaka 20. Kwa mara ya mwisho, hilo lilitokea mwaka 1976, kwenye michuano ya Olimpiki, wakati mabondia wa Marekani walitwaa medali tano za dhahabu, ikiwemo ya bondia nyota wa wakati huo, Sugar Ray Leonard.

Katika hatua ya nusu fainali ya kuwania medali ya shaba fedh dhidi ya Serafim Todorov wa Bulgaria, Mayweather alipoteza pambano kwa maamuzi ya utata kama ilivyokuwa kwa Roy Jones Jr.'s decision.

Kocha wa Marekani Gerald Smith alikata rufani, akilalamika kuwa, Mayweather alipiga ngumi, lakini hazikuhesabiwa, wakati Todorov aliongezewa pointi bila ya kurusha ngumi.

"Majaji walitoa hukumu kama inavyostahili," alisema Waeckerle. Majaji walishindwa kupunguza pointi mbili Todorov baada ya kufanya makosa mara tano.

"Kila mmoja anajua Floyd Mayweather, alikuwa bondia mwenye medali ya dhahabu katika uzito wa kg5 7," alisema Mayweather.

Mayweather alianza pambano lake la kwanza la ngumi za kulipwa Oktoba 11, 1996, dhidi ya Roberto Apodaca, na kumtwanga katika mzunguko wa pili.

Wakati huyo, kocha wake alikuwa mjomba wake Roger Mayweather, kwasababu Floyd Mayweather, Sr. alikuwa bado gerezani, baada ya kukamatwa na madawa ya kulebya mwaka 1993.

Mayweather, Sr. alichukua nafasi ya kumfundisha Mayweather, Jr.'s , baada ya kutoka gerezani, wakati huo mtoto wake tayari alikuwa amepanda ulingon mara 14, mara mbili akiibuka na ushindi wa mapema. Mwaka 1996 na mapema mwaka 1998, Mayweather alishinda baadhi ya mapambano kwa knockout au TKO.

Mayweather alikuwa bondia wa kwanza wa Marekani kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1996, nambapo promota wake Bob Arum alisema: "Tunaamini kutoka moyoni kuwa, Floyd Mayweather ni bondia anayefuata nyayo za Ray Robinson, na kufuatia Muhammad Ali, baadaye Sugar Ray Leonard," alisema Bob Arum.

Baada ya kutwangana na Gatti, Mayweather alihamia uzito mwingine, ambapo Novemba 19, 2005, alipigana na Sharmba Mitchell, pambano ambalo halikuwa la kuwania mkanda.

katika mzunguko wa tatu, Mayweather alimtwanga kwa Ko Mitchell kwa ngumi ya kulia iliyotua kichwani na kumpeleka chini, na katika raundi ya sita alimpiga tena Mitchell ngumi nzito iliyomta mchezoni na kumaliza pambano.

Aprili 8, 2006, Mayweather alimpiga Zab Judah na kutwaa mkanda wa IBF wa uzito wa welter. Kabla ya hapo, the fight baada ya Judah kupoteza mikanda yake ya WBA na WBC, lakini kambi ya Mayweather na Judah, waliingia makubaliano ya kuchapana makonde.

Mayweather katika pambano hilo alishinda kwa pointi 116–112, 117–111, na 119–109,ikionesha alirusha ngumi mara 188 dhidi ya 82 za Judah.

Siku tano baada ya pambano, Mamlaka ya ngumi ya Nevada iliamua kumpiga faini Roger Mayweather ya dola 200,000 na kumsimamisha kushiriki ngumi kwa mwaka mmoja.

Kusimamishwa kwake, kulikuwa na maana kuwa, Roger atakuwa akimfundisha Mayweather, Jr. katika gym, lakini hataruhusiwa kuwa katika kona ya bondia wake.

Bingwa mara saba, Manny Pacquiao iliripotiwa kuwa, yupo tayari kutwangana na Mayweather Machi 13, 2010, kwa kitita cha dola 50 milioni, huku mapromota wote wakikubaliana na hilo.

Pambano hilo halikufanyika baada ya Floyd Mayweather kutaka wapimwe damu zao kuchunguza matumizi ya dawa, lakini kambi ya Pacquiao ilikataa, na kuweka masharti kuwa,l itawezekana kama watapimwa kwa kuchukuliwa damu wiki moja kabla ya pambano.

Kwa hiyo, Januari 7, 2010, promota wa Pacquiao, Bob Arum alisema pambano hilo halitafanyika na kutoa nafasi ya kwa Pacquiao na Joshua Clottey, wakati Mayweather alikubali kupigana na Shane Mosley.

Julai 26, 2010, Ross Greenburg alisema katika taarifa yake kuwa, alizungumza na wawakilishi wa pande zote mbili tangu Mei 2, 2010, lakini pande zote mbili hazikuafikiana. Floyd Mayweather Jr., baada ya makubaliano ya mara ya pili kuvunjika, aliiambia Associated Press kuwa, alijua siku 60 kabla, hivyo hakuwa na mawazo ya kupigana na Pacquiao na hafikirii ngumi tena kwa wakati huo.

Mwaka mmoja baadaye, Julai 8, 2011, Manny Pacquiao, mshauri wake mkubwa Michael Koncz, alithibitisha kuwa, Pacquiao hakuwa tayari kuchunguzwa damu yake mpaka hivi sasa, kitu kilichoonekana kuwa, tofauti kwa Bob Arum na kambi ya Pacquiao, ilivyokuwa ikisema karibu mwaka wote.
Juni 7, 2011, Mayweather, aliatangaza kwenye mtandao wa Twitter kuwa, atawania mkanda wa WBC katika uzito wa Welter dhidi ya Victor Ortiz Septemba 17, 2011. Ortiz lilikuwa chaguo la kwanza la Mayweather katika miezi 16.

katika pambano hilo, Mayweather salimtwanga Ortiz na kutwaa mkanda huo.

Makala haya yameandaliwa na Frank Balile kwa msaada wa mitandao mbalimbali, kama unahitaji historia ya mchezaji yoyote wa kimataifa, tutumie ujumbe mfupi wa maneno, 0713 405 652.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...