Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 14, 2011

oma ya pambano wa Krismasi: Msondo wajichimbia Mwanza, Sikinde Dar


Na Mwandishi Wetu
Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya pambano baina ya bendi mbili zenye upizani mkubwa nchini, Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde), tayari bendi hizo zimeamua kupiga kambi kujiaanda na pambano hilo litalofanyika siku ya Krismasi kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.
Habari za uhakika zilizopatikana jijini Dar es Salaam zimebainisha kuwa bendi ya Msondo Ngoma imeweka kambi yao jijini Mwanza wakati wapinzani wao, Sikinde, wenyewe 'wamejificha' jijini Dar es Salaam kujiaandaa na pambano hilo linalofanyika chini ya udhamini wa kinywaji cha Konyagi.
Meneja wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Kibiriti, jana alithibitisha habari za bendi yake 'kuhamia' jijini Mwanza akisema kuwa wameamua kujichimbia mbali ili kujiandaa vyema na pamabano hilo ambalo hufanyika kwa nadra.
“Litakuwa ni pambano kubwa mno na muhimu kwetu" alisema Kibiriti na kuongeza; "inatulazimu tujiandae vyema ili tusije tukaangusha wapenzi wetu. Tumeamua kwenda Mwanza kwa sababu ni sehemu tulivu ya kujiandaa. Tukirudi Dar es Salaam kazi itakuwa moja tu, kuwashinda watani wetu.”
Naye afisa mipango wa Sikinde Hamisi Mirambo alisema wao watabaki jijini Dar es Salaam na kufafanua; “sisi hatuendi mbali, tutajificha hapa hapa jijini kutayarisha nyimbo zetu mpya ambazo tutazitumia kuwaangamiza wapinzani wetu,” alisema Mirambo.
Mpambano huo utakaoanza saa nane mchana hadi usiku, umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi chini ya uratibu wa Joseph Kapinga aliyetamba kuwa pambano hilo litakuwa la 'funga mwaka'.
Kapinga amesema mbali ya kutoa burudani kwa wapenzi wa bendi hizo mbili, pambano hilo pia litaamua ni ipi bendi bora ya mwaka 2011 kati ya bendi hizo mbili.
Ili kuondoa hisia za hujuma, hasa kwenye upangiliaji wa milio ya vyombo, kila bendi itatumia jukwaa lake kwa kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...