Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 31, 2011

WADAU WAOMBWA KUISAIDIA TWIGA STARS


Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia baadaye mwezi ujao.
Mechi hiyo ya kwanza itachezwa ugenini Januari 14 mwakani jijini Windhoek. Timu hiyo ambayo sasa inafanya mazoezi kwa wachezaji kutokea majumbani (off camp) inatarajia kuingia kambini Januari Mosi mwakani.
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linahitaji zaidi ya sh. milioni 50 ikiwa ni gharama za safari, kambi na posho kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya mechi hiyo moja tu. Mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...