Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 8, 2011

Wateja Vodacom M-PESA sasa kupokea pesa kutoka nje ya nchi kupitia huduma ya Western Union


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya pamoja na kampuni ya Western Union ambapo wateja wa simu za mkononi wa Vodacom nchini watakuwa wakipokea pesa kutoka nje ya nchi moja kwa moja kwa kutumia huduma ya Vodacom M-PESA,kulia Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Western Union wa Afrika mashariki na kusini Karen Jordaan.
Kampuni ya Western Union na Vodacom Tanzania zimezindua huduma mpya ambapo kuanzia sasa wateja wa Vodacom Tanzania watapata pesa zao kupitia huduma ya M-PESA. Kwa mara ya kwanza wateja wa simu za mkononi wa Vodacom nchini wanao uwezo wa kupokea pesa kutoka nje ya nchi moja kwa moja kupitia huduma ya Vodacom M-PESA. Huduma ya Mobile Wallet ambayo ndio itakaoyotumika kuwaunganisha wateja wa Western Union na M-PESA ni ya haraka, kuaminika na uhakika kwa marafiki na wanafamilia kutuma fedha kutoka nje ya nchi. Mtumaji anachopaswa kufanya ni kufika kwa mmoja kati ya mawakala 108,000 wa Wetsern Union katika nchi zaidi ya 65 ulimwenguni kote na kutuma pesa hizo ambazo zitatumwa moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mpokeaji ambaye ni mteja wa Vodacom M-PESA. Mpokeaji wa fedha hizo atatumiwa ujumbe wa kumjulisha kuingia kwa pesa hizo katika akunti yake ya M-PESA na kwamba ataweza kuzitoa pesa hizo kupitia moja ya wakala zaidi ya 15000 wa M-PESA kupitia taratibu za kawaida za utoaji pesa. "Siku zote Vodacom hutafuta suluhisho la mahitaji ya wateja wake kupitia huduma bunifu kama hii ambayo tunaizindua leo"Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza. Matumizi ya M-PESA yanaongezeka mwezi hadi mwezi na kumekuwepo kilio kutoka kwa wateja wetu wakitaka huduma hiyo kuvuka mipaka ya nchi, kilio ambacho tunafuraha kuona leo tumekipatia suluhisho kutoka M-PESA pekee. Kuanzia leo wateja wa M-PESA wanaweza kupokea pesa kutoka kwa ndugu na jamaa wanaoishi nje ya nchi ikiwemo Kenya na Uganda "Hakuna gharama zozote za ziada katika kuchukua pesa hizo kutoka kwa wakala zaidi ya gharama za kawaida za utoaji wa pesa."Aliongeza Rene Vodacom M-PESA ilizinduliwa mwaka 2008 na sasa ina wateja zaidi ya milioni tisa ikifanya miamala zaidi ya milioni moja kwa siku na ni huduma ambayo ni chagua la kwanza kwa wananchi katika kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo mbalimbali ikiwemo huduma za maji na umeme, kuongeza salio, kulipa kodi, kununua tiketi za ndege n.k. Western Union inaendelea kutoa huduma bora ikiwa kampuni inayoongoza katika huduma za utumaji wa pesa kutumia miundombinu yake iliyoenea ulimwenguni kote ikiwa na vituo zaidi ya 108000 katika nchi 65 na mikataba ya kibiashara na makampuni ya simu zaidi ya kumi duniani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...