Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 17, 2011

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI TUZO ZA SUPERBRADS KWA MAKAMPUNI YALIYOFANYA VIZURI MWAKA 2011,


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Super Brands, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni wa Simu za mkononi Vodacom, Mwamvita Makamba, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi tuzo hizo kwa Makampuni yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2011, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Superbrands, Jawad Jaffer (kulia) ni Ofisa Matangazo wa Vodacom, Joseline Kamuhanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Super Brands, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Fm, Joseph Kusaga, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi tuzo hizo kwa Makampuni yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2011, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Super Brands, Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Ephraem Mafuru.
TBL wakipokea Tuzo hiyo kwa pamoja.
Joseph Kusaga, akitoa neno la Shukrani baada ya kupokea tuzo hiyo.
Mwamvita Makamba, akitoa neno la Shukrani baada ya kupoea Tuzo hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Super Brands, Meneja Masoko wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Simon Marwa, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi tuzo hizo kwa Makampuni yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2011, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Superbrands, Jawad Jaffer. (kushoto) ni Emmanuel Matondo (kulia) ni Tonny Madatta.
Wanamuziki wa Bendi ya Borabora Sound, wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
Msanii wa Kundi la Wanne Star, akitoa burudani ya aina yake ambapo aliwasha Sigara kwa kutumia miguu na kisha kuivuta kwa miguu.
Hapa akianza kuivuta kwa kuishika kwa miguu.
Baadhi ya warembo waliokuwa wakitoa huduma katika ukumbi wa shughuli hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...