Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 1, 2010

URENO HAIKUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA

Na alice ngubwene
kama kawaida ureno nayo imefungasha virago kama timu zingine baada ya ya kupigwa bao moja bila na timu ya hispania.
Pamoja na kuingia kwa kishindo katikano hatua ya pili ya mashindano hayo Woza WC2010, ureno imeshindwa kuonyesha cheche zake na kuishia kuonyesha mchezo usiovutia kwa kushindwa pia kumfanya mshambuliaji wao kinara Christiano Ronaldo ang'are katika mashindano hayo kwa kukosa kuwa mpachika mabao bora kama alivyozoeleka akitokea klabu yake ya zamani ya Manchester united.

Ukilinganisha na vijana wa Vicente DeleBosque ambao baada ya kushtukizwa na kipigo cha goli moja kutoka kwa waswisi, hispania walijitahidi kuonyesha kiwango tofauti katika mechi zake zilizosalia katika mashindano hayo huku kinara wao wa kupachika magoli David villa aking'ara.

Timu zote zinajifunza kutokana na makosa kadri mashindano yanavyoendelea kupamba moto. Lakini haikuwa hivyo kwa vijana wa Quieroz ambao walionyesha udhaifu huo katika mpangilio wawapo uwanjani. ni aibu kidogo kwa wachezaji wa ureno ambao waliingia kwa kishindo katika mtoano wa raundi ya pili. Mechi hiyo na hispan ilianza kwa kasi nzuri ambapo vijana Del Bosque kina Torres na Villa wakipeleka mashambulizi maakali ambayo yaiokolewa na kipa wa ureno Eduardo.

Ukiangalia vema utagundua kuna tofauti kubwa kati aina ya uchexzaji na ubora ulioonyeshwa na hispania ukilinganishwa na wachezaji wa hispania. Hata kocha Dunga wa Brazil naye alijaribu kuwasema wareno kuwa walionyesha uchezaji ambao ni wa uzuiaji zaidi na sio wa kufurahisha!! ni mchezo ambao umeanzishwa na "the Special one" kocha wa baadaye wa ureno kwa asilimia 99 wa kuweka bus golini kama waingereza wasemamavyo, ingawa yeye anapinga hilo. mchezo huo ulionyeshwa zaidi na wachezaji wa ureno haukufurahisha na kufanya mchezo usiwe na mvuto na kasi yoyote!

Lakini pamoja ukuta uliowekwa na wachezaji wa ureno David villa alifanikiwa kuwadhihirishia kuwa yeye ni mshambuliaji mwenye uchu wa magoili wakati wote pale alipoipatia timu yake goli zuri baada ya kupokea pasi nzuri upande wa kushoto kutoka kwa mchezaji mwenzie na kuwezesha mabingwa hao wa ulaya kutoka kifua mbele na kuwavusha kuingia katika hatua ya robo fainali

Sawa Kocha wa ureno na wachezaji wake wanastahili kupata pongezi kwa kiwango chao cha uzuiaji lakini ingefurahisha kama wangeonyesha mchezo huo kama tayari wangelikuwa na mabao ya kutosha kuyalinda, tatizo lao walikuwa wanalinda hewa maana hawakuwa na chochote!

kwa maoni zaidi wasiliana na 0733 660669

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...