Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 1, 2011

BANZA APOKELEWA RASMI EXTRA BONGOMKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, maarufu kama Next Laver, Ally Choki, amesema kwamba sasa mambo yamezidi kuwa mazuri ndani ya bendi yao kutokana na uwepo wa Ramadhan Masanja, maarufu kama Banzastone.

Juzi katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama, bendi hiyo ilimtambulisha rasmi gwiji huyo na kuachia wimbo wake mpya, uliokwenda kwa jina la ‘Watu na Falsafa’.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Choki alisema kwamba mipango inaendelea ya kuhakikisha wanazidi kufanya vyema katika kona ya muziki wa dansi nchini.

Alisema uwepo wa Banzastone na wakali wengine ni harakati za kuwaweka juu katika ramani ya muziki huo unaozidi kuchanja mbuga hapa nchini.

Nashukuru kwa kiasi kikubwa uwepo wa wanamuziki wenye uwezo, akiwamo Banzastone, maaurufu kama Roho ya Paka au mwalimu wa walimu.

“Ana uwezo wa kutisha, kwani nyimbo zake na sauti yake ni dalili tosha kwamba yeye ni bora na mashabiki wetu watafurahia kazi zake akiwa hapa Extra Bongo,”alisema.

Banzastone amejiunga na bendi hiyo na kuungana na Choki, Rogati Hega Katapila, Saulo John, Ferguson .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...