Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 19, 2011

MISS CHANG'OMBE 2011 APATIKANA USIKU HUU TCC CLUB


Miss Chang'ombe 2011 Sinsia Kamasha akipunga mikono kwa maswhabiki wake mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Miss Chang'ombe lililomalizika usiku huu kwenye viwanja vya klabu ya TCC Chang'ombe jijini Dar es salaam, kushoto ni Husna Twalib mshindi wa pili na kulia ni Joyce Mawega Kumbuka Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel ni Miss Chang'ombe pia hivyo leo anayo kazi ya kuvua taji lake la kwanza katika shindano hili la Miss Chang'ombe mara atakapotangazwa Pappa-zi Miss Chang'ombe usiku huu.
Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude akikabidhi zawadi ya shilingi laki tatu iliyotolewa kama nyongeza kwa washindi kutoka kampuni ya Pappa-zi Intertainment
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya usambazaji wa kazi za wasanii hapa nchini Pappazi-Intertainment Zakaria Hanspoppe akikabidhi zawadi ya dola 500 ambayo kampuni yake hiyo imetoa ili kuongezea mzawadi. Husna Twalib mshindi wa pili
Washiriki walioingia kwenye tano bora wakipabana kwenye maswali kabla kutangazwa kwa Miss Chang'ombe 2011.
Hapa ni Washindi walioingia katika tano bora ya shindano la Pappa-zi Miss Chang'ombe 2011 linalofanyika usiku huu kwenye viwanja vya TCC Sigara jijini Dar es salaam kumekuwepo na utulivu na warembo wamejaribu kufanya kila linalowezekana kwa kufuata kanuni za mashindano ili kuweza kuibuka na ushindi katika shindano hilo.
Vazi la ufukweni ndiyo hili hapa.
Ubunifu huu nadhani umetukuka kwani mpaka mguu umepata kipande chake cha nguo.
Vazi hili limebuniwa kwa kutumia khanga.
Hapa wakiwa katika vazi la ubunifu.
Vazi la ubunifu hilo hapo.
Warembo wanaoshindana katika shindano la Miss Chang'ombe jijini Dar es salaam usiku huu wakiwa jukwaani kwa shoo ya ufunguzi wa shindano hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa Pappa-zi Entertainment Zakaria Hanspope akifungua rasmi shindano la Miss Chang'ombe usiku huu.
Kutoka kulia ni wanamuziki wa bendi ya muziki wa dansi ya Mapacha Watatu Kalala Junior, Jose Mara, na Harid Chokoraa wakifanya vitu vyao jukwaani..
Kundi la Mapachja Wat.atu wakiwa katika shoo kali usiku huu katika shindano la Miss Chang'ombe usiku huu
Mashabiki mbalimbali wakiwa katika shindano la Papaazi Miss Chang'ombe linalofanyika usiku huu kwenye viwanja vya TCC Sigara jijini Dar es salaam.
http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...