Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 1, 2011

MASHABIKI WA MAN U WAJIFARIJI NA MWENDELEZO WA MSIMU WA DHAHABU WA SERENGETI


Timu ya mashabiki wa timu ya Manchester United ya uingereza ambao wameibuka kidedea na kuwa mabingwa katika Tamasha la mabingwa wa Mwendelezo wa Msimu Dhahabu na Serengeti Soccer Bonanza Mkoani Tanga, wakishangilia na kuinua kombe lao juu baada ya kushinda katika mchezo dhidi yao na timu ya mashabiki wa Barcelona mkoani humo na hatimaye timu hiyo ikamalizia hasira zake kwa wapinzani wao hao Barcelona kwa kuwabamiza kwa mikwaju ya penati tatu kwa moja baada ya kutoka suluhu katika dakika za 90 kumalizika bila kufungana kwenye bonanza lililofanyika leo kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Meneja mauzo wa Kampuni ya Serengeti Breweries mkoani Tanga, Faki Mohamed,(mwenye kofia) akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya mashabiki wa Manchester United, Julius Silasi, baada ya timu hiyo kuibamiza Barcelona katika mchezo wa fainali za Mwendelezo wa Msimu Dhahabu na Serengeti Soccer Bonanza. Kulia ni mratibu wa Bonanza hilo, Shafii Dauda (katikati) ni Meneja Mauzo wa Kanda Patrick Kisaka na Peter Ngassa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...